Pages

Pages

Tuesday, December 04, 2012

Mwandishi wa Mtanzania awania tuzo



 Mohamed Mharizo, pichani.

Na Kambi Mbwana
MWANDISHI wa gazeti la Mtanzania, Mohamed Mharizo, ni miongoni mwa wanaowania tuzo ya ‘Fashion Journalist of the Year 2012’, inayoandaliwa na Swahili Fashion Week, chini ya mbunifu mahiri Afrika Mashariki na Kati, Mustafa Hassanali.

Kufuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika tuzo za mwaka jana, Tuzo za Swahili Fashion Week 2012 zinazoendana na kusherehekea miaka mitano tangu kuzaliwa kwa onyesho hili kubwa la mitindo Afrika Mashariki na Kati mwaka huu, zimeongezwa tuzo nyengine tatu kutoka katika tuzo za mwaka jana ili kuweza kutoa changamoto kubwa zaidi katika tasnia ya mitindo hapa nchini na Ukanda wote wa Afrika Mashariki na Kati. 

Hivyo kufanya jumla ya tuzo 15 kuwaniwa mwaka huu kutoka tuzo 12 za mwaka jana.

Tuzo za mwaka huu ni: Best Male Model, Best Female Model, Best East African Model (Mpya), Designer of the Year, East African Designer of the Year, Redd’s Stylish Female Personality, Stylish Male Personality, Innovative Designer, Best Men’s Wear, Fashion TV Program of the Year (Mpya), Vodacom Fashion Blog of the Year, Fashion Photographer of the Year, Fashion Journalist of the Year, Best East African Journalist (Mpya) na  Upcoming Designer.
Ili kumpigia kura Mharizo, tuma ujumbe was ms kwa kuandika SFWAFJ05 kwenda 15678.

Wengine wanaowania tuzo hiyo ni Maimuna Kubegeya (Mwananchi), Evance Ng’ingo (Habari Leo), Dina Ismael (Tanzania Daima), Giver Meena (Bang Magazine), na Masembe Tambwe (Daily News).

Mchakato mzima wa kuchagua mwanamitindo na mbunifu wako bora kwa mwaka huu wa 2012 unasimamiwa na PUSH Mobile, ambapo mpiga kura atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wa namba ya mshiriki (CODE) unaemkubali na kwenda kwenye namba 15678.
Pia kura zinaweza kupigwa kupitia blogu maalum ya kupigia kura ya www.sfw2012awards.blogspot.com

Washindi wote wa Tuzo za Swahili Fashion Week 2012, watatangazwa siku ya ya mwisho ya Maonyesho ya Swahili Fashion Week, Jumamosi ya Desemba 8, 2012 katika hoteli ya Golden Tulip, Dar es Salaam, Tanzania. 

Swahili Fashion Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila mwaka kati.

Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na: Vodacom, USAID Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula, Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites, Ultimate Security, BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania), Strut It Afrika, Ndibstyles, PKF Tanzania, DARLING, PUSH Mobile, DarLife, Century Cinemax and 361 Degrees.

No comments:

Post a Comment