Pages

Pages

Sunday, December 16, 2012

Mvuto wa Wema Sepetu ni balaa kwa wanaume


Wema Sepetu ndio huyu sasa

Na Mdakuzi wetu
Licha ya kuandikwa sana katika vyombo vya habari na wakati mwingine habari mbaya kwake, lakini msanii wa filamu na mrembo wa zamani wa Miss Tanzania, Wema Sepetu, ameonekana kuwa na mvuto unaochanganya wengi.

Wema ambaye kwa sasa wanaendeleza uhusiano wake na Diamond kwa siri kubwa, sura yake inauza kiasi cha kuwafanya waandishi wamsake kila wakati, huku wasanii na watu wengine kutaka ukaribu nae.
 Silaha ya Wema magazeti

Uchunguzi uliofanywa na Handeni Kwetu, umegundua kwamba kati ya watu waliokuwa kwenye uhusiano na mwanadada huyo, wamefanikiwa kujenga majina yao na kufanya vyema katikaa kazi zao.

Miongoni mwa watu hao ni Fresh Jumbe, Chalz Baba, Steven Kanumba, Diamond ambao ingawa walikuwa wakijulikana, lakini umahiri na majina yao yalizidi kuchanua katika uhusiano na malkia huyo.

Jambo hilo lilisababisha watengenezaji wa bia ya Serengeti, wabuni wazo la wasanii wa filamu akiwamo Ray, Wema, Steve Nyerere na JB wazunguuke katika mikoa mbalimbali katika shoo ya Fiesta.

Katika mikoa yote, Wema alionekana kunogesha zaidi shoo hizo, huku akiacha watu wakiwa kwenye pilika pilika nyingi, wakionekana kupagawa juu ya haiba na mwonekano wa mrembo huyo wa zamani wa Tanzania.

Mashabiki wa filamu na muziki watambuka shoo ya mjini Dodoma, pale Wema alipoonekana jukwaa moja na Diamond, jambo ambalo lilizidi kumng’arisha kijana huyo aliyekulia maeneo ya Tandalee.

Kwa sababu hiyo, kuna kila sababu ya kusema kuwa mvuto wa Wemaa ni mkubwa kiasi cha kuweza kumpa umaarufu mtu yoyote atakayeweza kuwa na uhusiano na malkia huyo anayemng’aa kwa miaka kadhaa sasa.

Huyo ndiye Wema Sepetu

No comments:

Post a Comment