Pages

Pages

Thursday, December 13, 2012

LADHA ZA WASANII WETU



 Diamond anaposema ‘Nalia’
Diamond pichani

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NAKUKARIBISHA mdau wa Handeni Kwetu katika kona hii mpya ya kuchambua mashairi ya nyimbo mbalimbali za kizazi kipya kwa ajili ya kutuelimisha na kuburudisha pia.
 
Leo tuanze na wimbo wake Diamond unaokwenda kwa jina la 'Nalia', aliyoimba sambamba na mkali wa Hip Hop hapa nchini, namzungumzia Chid Benz.

Ni wimbo wenye mashairi mazuri, huku yakiimbwa kwa ubora wa hali ya juu. Najua mashairi haya yatakukuna kisawa sawa, maana yanagusa mapenzi.

Diamond katika kibao hiki anasema anajua mapenzi ni kama bahari, kamwe haina utani. Anasema unapozama kwenye bahari, kupotea ni kwa asilimia kubwa, hata kama uwe unajua kuogolea zaidi ya samaki.
 Diamond enzi za uhusiano wake na Wema Sepetu

Huyo ndiyo Diamond bwana. Amekuwa makini mno katika kutunga na kuimba vibao vya mapenzi. Mwanadada Wema Sepetu, aliwahi kuieleza kona hii kuwa hata kama ameachana na msanii huyo, kamwe hatachoka kuwa shabiki wa jamaa huyo kwa madai kuwa anazimikia nyimbo zake.

Wema anajua kuwa ni vibao maridadi vyenye ujumbe mzito katika mambo ya mahabati, ndio maana anashindwa kuzizuia hisia zake.

Diamond anasema ndani ya wimbo huu kuwa mapenzi yanatesa na kuumiza vibaya. Kama hivyo ndivyo, basi yeye amemuumiza zaidi mwadada Wema, hasa pale alipokataa pesa zake katika moja ya shoo zake, iliyofanyika Mlimani City.

Ni wakati wetu sasa kuangalia kwa kina mapenzi kwa kuhakikisha kwamba tunakuwa na watu wenye  mapenzi ya kweli na sio wale matapeli.

Haya ndio mashairi ya wimbo huu.

Diamond

Me niliambiwa mapenzi ni kama bahari,
Ukishazama ndo basi umepotea,
Kumbe mwenzangu alikuwa na taa,
Badala ya kuzama me kwangu akaelea
Akawa ananidanganya nikiwa nadhani ananipenda sana
Mikwanja nikamwaga mama, japo sio kivile
Akawa ananidanganya nikiwa nadhani ananipenda sana
Mbona mifedha nikamwaga mama,
Japo sio kivile Wakaja wajinga wakamchukua
Wakamhonga honga mwisho wakamnunua
Wajinga wakamchukua, wakamhonga honga mwisho wakamnunua yaya haaaa

Kiitikio

Usinione nalia usinione nalia mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia nalia sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia nalia nalia na mengi
Uuuhhhh jamani nalia nalia sababu ya mapenzi

Ubeti 2

Najua alimaanisha kuwa simfai ila lakini angesema
Kuliko alichofanya me akantoa nishai akanimeza akanitema
Nyie mapenzi yanauma vibaya vibaya vibaya
Mmmmhhhhh mapenzi yanauma vibaya vibaya vibaya
Safari ndo inanifanya mi usingizi sipati
Huwa nakumbuka mbali hasa nikisikia harufu yake ya marashi
Kwa uchungu nilivyoumia katika hili songi
Nalia, nafuu kwa hisia naimani iko siku nyimbo itamfikia
Me kwa uchungu nilivyoumia mie katika songi
Nalia, nafuu kwa hisia naima ni iko siku nyimbo itamfikia
Yayayaaa

Kiitikio
Usinione nalia usinione nalia mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia nalia sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia nalia nalia na mengi
Uuuhhhh jamani nalia nalia sababu ya mapenzi

Chid Benz

Usione nakosa raha mama nalalama kwako mara kadhaa
We ni msaada kwenye tuta so ukichomoka balaa
Sijiwezi kwangu giza naweza kimbiza na hii taa
Na hilo unajua inavyoumiza ushashuhudia mara kadhaa
Wezi wakung'ang'anie ninung'unike nilie
Njia yetu moja niache nipite si ukasimulie
Ya kinyamwezi na swaga zako juu
Na miguu napata picha kitandani kungfu
Uko juu ukipita lazima wasome namba
We ndo kibri fimbo kiboko ya midomo mamba
Huu ndo mfano hata unajua neno pamba
Kwa kitambo ntakulinda kama mkinga mwenye shamba
Mikogo kila leo ntajigamba, kisela piga teke inauma
Usiombe mapenzi yakupige teke inauma
Usiombe mapenzi yakupige teke eee

Kiitikio

Usinione nalia usinione nalia mwenzenu nalia na mengi
Usinione nalia nalia sababu ya mapenzi
Mwenzenu nalia nalia nalia na mengi
Uuuuhhhh jamani nalia nalia sababu ya mapenzi

0712 053949
0753 806087

No comments:

Post a Comment