Pages

Pages

Thursday, December 27, 2012

Chagga Day laungwa mkono Moshi, Kilimanjaro

 DJ akionyesha manjonjo yake Chagga Day

 Picha mbalimbali za burudani ya Chagga Day Moshi



Ommy Dimpozi, akitoa shoo Chagga Day Festival

Na Mwandishi Wetu, Moshi
TAMASHA la Chagga Day Festival limefanyika kwa mafanikio makubwa katika Ukumbi wa Zumba Landa, uliopo Moshi, Desemba 22, huku waandaaji wakifurahia na kuwapongeza wadau wote waliofanikisha shughuli hiyo.

Tamasha hilo kwa ujumla lilipendeza huku likiandaliwa na kampuni hiyo ya burudani kwa ajili ya kuwapatia burudani kamili watu wa huko sambamba na kuenzi mila na destuli za kabila la Wachaga walioenea katika mkoa huo.

Mkurugenzi wa Kampuni ya My Way Entertainment, Paul Maganga, aliwapongeza mashabiki na wadau wote waliohudhuria kwa wingi kwenye tamasha hilo la Chagga Day Festival, ambalo ni mwendelezo wa lile la kwanza la Chagga Day Cultural Festival 2012 - Dar lililofanyika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam miezi miwili iliyopita.

Tamasha hilo lilipambwa na burudani ya muziki wa dansi toka kwa Serengeti Band yenye maskani yake jijini Arusha, pamoja na kundi la madansa la Boda 2 Boda, bila kusahau nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz.

Tamasha hilo lilidhaminiwa na TBL, TDL na SBC ambapo TBL ni kupitia bia ya Safari na SBC wakisherehesha kupitia soda za PEPSI na TDL kupitia Konyagi.






No comments:

Post a Comment