Pages

Pages

Sunday, December 16, 2012

CCM Handeni waendeleza tambo zao


 Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Mrisho Kikwete, akipeana mikono na watoto, katika moja ya shughuli za kichama.

Na Rahimu Kamb, Handeni 
MWENYKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Handeni mkoani Tanga, Athumani Malunda, amejigamba kuwa wilaya yao itaendelea kuwa ngome imara ya chama chao kutokana na wananchi wao kuwaheshimu na kukithamini na kukiweka madarakani.

Malunda aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini hapa, akizungumzia pia mikakati ya chama katika kusimamia watendaji wao kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa Handeni na Tanzania kwa ujumla.

Akizungumza na Handeni Kwetu, Malunda alisema kwamba historia inaonyesha kuwa wilaya yao ni ngome imara ya CCM, hivyo uongozi hauwezi kukubali kuiondosha sifa hiyo muhimu kwa Taifa lao.

Alisema CCM Handeni na Taifa kwa ujumla watashiriki kwa karibu kuwakumbusha viongozi wao kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wananchi wao wanapata maisha bora jambo litakalowapa imani zaidi.

“Tanzania imekuwa ikikabiriwa na siasa za vyama vingi lakini kwetu tunashukuru kuwa wananchi wetu ni waelewa zaidi na wanakipenda chama chao, ndio maana hivyo vyama vya upinzani havina nguvu hapa kwetu.

“CCM imekuwa ikiongoza kwa mafanikio makubwa pamoja na kutatua kero za wananchi wao siku hadi siku, hivyo sioni sababu ya Handeni kuondoka kwenye utawala wa CCM na kuwaachia wapinzani, wasiojitambua na wasiokuwa na sifa ya kuwaongoza Watanzania, tukiwapo sisi Handeni,” alisema Malunda.

Maneno ya Malunda yamekuja katika kipindi ambacho baadhi ya Watanzania wamekuwa kwenye nafasi ngumu hasa kwa kuaminishwa kuwa CCM imeshindwa kutatua kero zao, hivyo wanastahili kuongozwa na wapinzani.


No comments:

Post a Comment