Mufti Mkuu wa Tanzania, Shabaan Simba
Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
UMOJA wa
Waadhir wa Kiislamu Tanzania, umesema kwamba mgogoro uliopo unatengenezwa na
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, ili waendelee kuuza mali za Waislamu.
Hayo
yamesemwa leo na Msemaji wa Umoja huo, Ustadh Said Juma Kinyogoly katika
kutangaza juu ya kuwathamini na kuwaunga mkono viongozi wao, waliopatikana
baada ya kufanya uchaguzi Novemba 20 mwaka huu.
Umoja huo
ulichukua uamuzi baada ya kudai kuwa wapo baadhi ya watu wanaopita katika
misikiti na kutangaza kuwa umoja huo haupo kihalali, jambo ambalo linaweza
kuibua mgogoro mzito miongoni mwa waislamu.
Akizungumza
mapema leo mchana, Msemaji wa Umoja huo, Kinyogoly, alisema kwamba BAKWATA
wamekuwa wakifanya mambo ambayo ni mabaya kwa waislamu.
Hawa
wamekuwa wakiuza mali za waislamu kwa faida yao, ukiwapo uwanja wa Markaz ambao
kesi bado ipo Mahakamani.
Na sio heka tatu
kama inavyojulikana, badala yake zipo heka 27 pamoja na nyumba mbalimbali
ambazo kwa pamoja ni mali ya waislamu,” alisema Kinyogoly.
Kinyogoly
pia alitumia muda huo kusema kuwa viongozi wao ni halali na wanaopita
wakitukana wanafanya hivyo kwa maslahi yao binafsi.
Umoja huo
upo chini ya Ustadh Habibu Mazinge aliyechaguliwa kuwa Amir Mkuu, Rajabu Juma,
alishinda nafasi ya Naibu Amir Mkuu, Juma Ramadhani, Katibu Mkuu, ambaye hata
hivyo alijitoa katika nafasi hiyo kutokana na kutingwa na mambo mengine, wakati
Rashidi Piringu yeye alichaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.
Wengine
walioshinda ni Mweka Hazina Mkuu, Hafidh Athuman, wakati Naibu wake ni Abdallah
Mazrui, huku Hussein Feruzi akichaguliwa kuwa msemaji wa umoja huo, ingawa naye
alijitoa, hivyo nafasi hiyo kubaki kwa Naibu wake, Kinyogoly.
Kwa mujibu
wa Kinyogoly, wanaopita kuwasema vibaya viongozi wao, wautumie pia muda huo
kuutetea uislamu pamoja na mali zake zinazouzwa kama njugu na viongozi kutoka
BAKWATA pamoja na wanaoshirikiana nao kuudhoofisha uislamu.
No comments:
Post a Comment