Pages

Pages

Tuesday, December 18, 2012

Baada ya kuanguka Arusha, Sajuki apewa kitanda Amana

MSANII wa filamu hapa nchini, Juma Kilowoko, maarufu kama sajuki, amepumzishwa katika Hospitali ya Amana, iliyopo Ilala, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia afya yake baada ya kuanguka jana, jijini Arusha.

Sajuki amepelekwa katika hospitali hiyo leo asubuhi kwa ajili ya kuangalia afya yake, ikiwa ni kutokana na matatizo yake ya tumbo yaliyosababisha apelekwe nchini India kwa matibabu zaidi, hasa baada ya kupata michango ya wahisani.

Msanii Sajuki alipoanguka jana jijini Arusha

Akizungumza na Handeni Kwetu jioni hii, Katibu wa Baraza la Filamu nchini (TAFF), Wilson Makubi, alisema hali ya Sajuki sio nzuri kutokana na maradhi yake yaliyosababisha apelekwe India hivi karibuni.

Alisema amepumzishwa katika hospitali hiyo kuangalia afya yake kwa ajili ya kumuweka katika mazingira mazuri msanii huyo ambaye alisababisha achangiwe kutokana na kukosa uwezo wa kifedha wa kumpeleka India.

Sajuki hadi muda huu yupo hospitali akiangaliwa afya yake na jinsi alivyopata maumivu baada ya kuanguka jijini Arusha jana katika shoo yake.

Tunamuombea kwa Mungu, huku tukiamini kuwa afya yake itaimarika ukizingatia kwamba anatarajia kurudi tena nchini India kupima kuangalia mwenendo wa matibabu yake," alisema.

Hata hivyo, Sajuki kwa siku kadhaa sasa amekuwa kwenye wakati mgumu akihangaikia namna ya kupata fedha za kumpeleka tena India, hasa wasanii wa filamu Bongo Movie kumuwekea ngumu kushiriki tamasha lake la Arusha.


No comments:

Post a Comment