Pages

Pages

Thursday, November 10, 2011

Mwanamke aliyeacha Jeshi kwa ajili ya sanaa


KELVINA JOHN

Mwanamke aliyeacha Jeshi kwa ajili ya sanaa

WAHENGA walikuwa na semi zao ambazo zilikuwa na maana sana. Kati ya hizo, upo ule wa ‘Umdhaniaye ndiye kumbe siye’, huu unastahili kabisa kupigiwa mfano kwa Kelvina John.

Je, unajua kwa nini mwandishi wa makala haya anatolea mfano wa usemi huo kwa Kelvina? Hiyo ni kutokana na kuamua kuvua gwanda za Jeshi la Wananchi Tanzania  (JWTZ) kwa ajili ya kujikita katika kucheza filamu, fani ambayo anaendeshea maisha yake kwa sasa.

Katika mahojiano, Kelvina alisema uamuzi wake huo ulitokana na uthubutu wake kwa sababu kazi hiyo ya kuwa muigizaji na mtengeneza (Prodyuza) filamu alikuwa akiipenda tangu utoto.

“Maisha ni kujaribu, inakupasa mtu kujaribu na hasa kwa kile unachokipenda na hakika utafanikiwa kwa sababu utakifanya kwa ufanisi wa hali ya juu, ndivyo ilivyojitokeza kwangu na kufikia uamuzi wa kuachana na kazi ya Jeshi na kujikita katika filamu.

“Ingawa nilipata wakati mgumu kuanzia katika Jeshi, lakini namshukuru Mungu hivi sasa nafanya kile ambacho nafsi yangu inapenda na naweza kuendesha maisha yangu kutokana na kazi hii ya kuandaa na kucheza filamu,” ndivyo alivyoanza kuzungumza Kelvina.

Kwa wasiomfahamu vema, Kelvina John ni muandaaji wa filamu (Prodyuza) ambaye alianza kujikita katika fani hiyo mwaka 2000 kwa kuandaa filamu yake ya kwanza kabisa ambayo aliamua kuiita Mtazamo.

Ingawa pia na yeye ni muigizaji, lakini anapenda zaidi kufanya kazi ya uandaaji, kazi ambayo hapa nchini imekuwa ikifanywa zaidi na wanaume  na ndiyo maana upo uwezekano mkubwa kabisa akawa ni mwanamke pekee aliyeamua kujiiingiza katika fani hiyo ya uandaaji.

Pengine ujasiri huo umetokana na kuwa mwajiriwa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ambaye alihitimu mafunzo na kupewa namba ya kazi 2712MTM na kupangiwa kazi katika kikosi namba 312 KJ Lugalo, kabla ya kuamua kuvua gwanda na kujikita katika filamu.

Katika mahojiano yake na Mtanzania, Kelvina alisema aliamua kuachana na kazi hiyo ya jeshi aliyoifanya kwa uadilifu ili akafanye kazi ya kuandaa na kuigiza filamu kwa sababu ni kitu kilichokuwa moyoni mwake tangu utoto.

“Ki ukweli katika maisha kila mmoja ana jambo ambalo anapenda, kwa sababu siku zote mimi nilikuwa naipenda fani hii, hata nilipokuwa jeshini nilihisi kama bado moyoni mwangu kuna jambo napungukiwa.

“Kwa sababu sikutaka kuidhulumu nafsi, niliamua ‘kusarender’ kazi ya jeshi na kuamua kujikita zaidi katika kuandaa filamu sambamba na kuigiza, kazi ninayoifanya hadi leo inayoniingizia kipato na kufanya nitatue matatizo yangu,” alisema.

Alisema aliamua kujitoa Jeshini mwaka 2003 baada ya kuona kazi yake ya kwanza aliyoandaa mwenyewe ambayo aliiita Mtazamo ikifanya vizuri, hivyo kuona ipo haja kutumia muda zaidi katika fani hiyo.

Kwa sababu inafahamika kazi hiyo ya Jeshi ni ‘bize’ sana kama angeendelea kuifanya, basi asingekuwa na muda wa kutosha kuandaa filamu zake, ndipo alipoamua kujivua gamba.

Mpaka sasa amefanikiwa kuandaa filamu tano, ikiwamo ambayo iko katika mchakato wa mwisho wa maandalizi ambayo inaitwa Leave or Die. Ni filamu ya action iliyowashirikisha mastaa kibao wa fani hiyo na kati yao mbali ya yeye mwenyewe, yupo Anti Fifi, Winter, Shilole na wengine.

Nyingine ambazo Kelvina amekwishatoa ni ile ya Penzi la Baba, Machozi na The Dadaz, ambayo aliitoa mwaka juzi. Aliwataka wanawake kuwa na uthubutu wa maamuzi ya mambo yao ili kufikia ndoto wanazohitaji, kwani hakuna lisiloshindikana endapo utakuwa na nia.

“Naomba wanawake wenzangu waache kubweteka, mimi unavyoniona dada yangu, naendesha maisha yangu kwa kazi hii, kwani imeniwezesha kuwapeleka watoto wangu wawili shule ambao Mungu amenijaalia.

“Na sasa nimeanza ujenzi wa kibanda cha kuishi huko jijini Mwanza, ambako ndiko ninapotokea, hivyo wale wenye mtazamo hasi juu ya kazi hii waachane nao kabisa,”  alisema.

Akizungumzia maisha binafsi nje ya shughuli hizo za uandaaji wa filamu pamoja na kuvua kwake gwanda za Jeshi, Kelvina anasema yeye ni mama wa watoto wa kike wawili aliobahatika kuwapata kati ya miaka minane iliyopita.

Hata hivyo, ilimlazimu kuachana na mumewe ambaye naye alitaka kumtia kiwingu kutokana na kutokubaliana naye kujihusisha na kazi hizo za uandaaji filamu, jambo ambalo hakukubaliana nalo ingawa awali alifanya hivyo.

“Kwa kweli hii ni sehemu ya changamoto katika maisha, namshukuru sana Mungu kuendelea kunipa ujasiri, hasa baada ya kupitia wakati mgumu na kufikia uamuzi wa kuachana na mume wangu ambaye hakuridhia nifanye kazi hii,” alisema.

Kwa sasa anaishi Mbezi jijini Dar es Salaam na ni mtoto wa kwanza katika familia yao ya watoto wanne, huku akiwa ndiye mtoto wa kike pekee. Akizungumzia ushirikiano anaoupata katika familia, alisema hakuna, kwa sababu hawafurahii fani aliyojikita.

“Baba yangu hataki hata kidogo nifanye kazi hii, yeye alitamani sana niwe ‘Air Hostess’ kwani ndiyo fani aliyonipeleka kusoma kabla ya mimi kuikacha na kujiingiza katika Jeshi, ingawa hakuvutiwa nayo sana, lakini aliipenda baada ya kusikia nimehitimu mafunzo na kuajiriwa.

“Nilikuja kumtibua tena nilipoamua kuvua gwanda na kujikita katika filamu. Simlaumu sana kwa sababu najua yeye, familia, ndugu na jamaa bado wana mtazamo hasi wa kazi ninayoifanya, lakini nataka niwaonyeshe kwamba sivyo wanavyofikiria.

“Ndio maana nahitaji kufanya mambo makubwa katika fani hii yatakayonifanya niwe msanii mkubwa ninayetambulika ndani na nje ya nchi na hapo nafikiri wataelewa nini nafanya na sasa nimeishaanza kuwaonyesha, hasa nilipofanikisha kumiliki kampuni yangu ya ‘Production’ ya kazi za filamu inayoitwa KJ Production,” alisema.

Kila kazi inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Je, unajua fani hii ya filamu inakabiliwa na changamoto gani?

“Changamoto kubwa tunazokabiliana nazo katika fani hii hapa kwetu ni kama tatu hivi: Sehemu za kuigizia, wasanii wengi ni wasumbufu, hasa baada ya kulewa sifa, hivyo kitu unachotakiwa kufanya siku mbili inaweza kuchukua hata wiki, soko la kazi zetu na tatizo la wizi wa kazi ni kubwa mno, tunaomba Chama cha Hakimiliki (COSOTA) kisimame imara, wasanii tunaumizwa sana hatufaidiki vilivyo,” alisema.

Ushauri wake kwa Serikali, watambue vema umoja wao waliounda unaoitwa Tanzania Films Federation (TAFF) na kuupa nguvu uweze kufanya kazi ipasavyo pengine utasaidia kuzuia wimbi la wizi wa kazi zao.

Lakini kwa upande wa wasanii wenzake, aliomba kujenga tabia ya kuheshimiana, kushirikiana na kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi kwa maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla. Huyo ndiyo Kelvina John.

xxxxxxMWISHO
 

Tuesday, November 01, 2011

Serikali izivunje COSOTA na BASATA

JUMATANO ya wiki hii nilikuwa miongoni mwa wadau wa sanaa waliohudhuria kikao cha Kamati ya Huduma za Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , kilichoongozwa na Mwenyekiti wake Jenista Mhagama.
 
Kikao hicho kilichohuduriwa pia na wasanii wa aina mbalimbali, kilifanyika katika viungwa vya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kikiwa na maana kubwa ya kujadili masuala mbalimbali ya sanaa na wasanii nchini.
 

                                          Waandishi wa habari wakiserebuka.
Kikao hicho kilikuja wakati muafaka. Wakati ambao kwa miaka kadhaa sasa, bado wasanii wamekuwa wakiishi maisha ya kubahatisha huku wengine wakiindelea kuishi maisha mazuri kwa kupitia migongo ya wasanii.
 
Mengi yalisemwa. Wasanii wengi walichangia pamoja na wajumbe ambao ndio wabunge na wageni waarikwa. Inasikitisha sana . Kwani kwa kiasi kikubwa, matatizo mengi yalihjitokeza, huku chanzo chake kikiwa ni BASATA na ndugu zao COSOTA.
 
Hata hao wezi wanaodaiwa kuwapo, ilionekana dhahiri wanabebwa na wakubwa wao, ukizingatia kuwa BASATA ina uwezo wa kuwa wakali kwa ajili ya kuwakomboa watoto wao, yani wasanii ambao kwa Tanzania wanaishi kama omba omba.
 
Licha ya kuwa na vipaji vya hali ya juu, lakini wanachopata ni sifuri. Ni kutokana na hilo , nadiliki kusema kuwa ipo haja ya Serikali, kupitia Wizara yake ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ili kuokoa maisha ya wasanii.
 
Kuvunjwa huko kunatokana na taasisi hizo kushindwa kufanya kazi zake kama inavyotakiwa, licha ya kupewa memo na wasimamizi wa sanaa kwa ujumla. Ndio, ingawa kwa COSOTA wao wanaweza kuyumba na msimamo wa Serikali, yani kuripoti kwa Wizara tofauti, kama ile ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
 
Pamoja na hayo, bado hainifanyi niamini kuwa COSOTA na BASATA wanaweza kukomboa maisha ya wasanii wetu. Kwa sasa uwezo huo hawana. Maana kwa miaka kadhaa wamekuwa wakifanya kazi kwa kuleana zaidi badala ya kusimama kwenye ukweli.
 
Angalia, ukweli huu umedhihirika zaidi, maana viongozi hao wa COSOTA waliweza kuingia mitini, japo walijua kuwa walitembelewa na Serikali yao , iliyowekwa madarakani kihalali, huku ikiongozwa na watu makini.
 
Jamani, hakuna haja ya kulumbana. Hapa hakuna haja ya kuogopana. Kwanini BASATA waachwe na ndugu zao COSOTA? Kwa wale waliokwenda katika mjadala huo watakubaliana na mimi. Malalamiko mengi yalielekezwa kwao.
 
Usimamizi wao ni mdogo zaidi. Kuingizwa katika biashara za kujinyoji hiyo ndio kazi yao , hata kama wanajua hazina umuhimu kwa Watanzania. Kwa mfano, BASATA kuingizwa kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award huo ni umbumbumbu.
 
Tuzo hizo zinayumba. Hazina maana. Wasanii bora wanaachwa na wale wabaya wanapata tuzo. Sasa kwanini washiriki? Hawaoni ni kuwayumbisha Watanzania? Haya ni maswali ambayo majibu yake ni rahisi, endapo viongozi watajivua gamba.
 
Hayo yatakwisha kama viongozi hao watakubali kuwajibika. Moja ya sera ya uongozi bora ni kusimama kwenye ukweli kwa ajili ya manufaa ya watu wako. Inapotokea mambo yanakwenda tofauti, huo ni wizi.
 
Tuuseme hadharani, maana vikao kama hivyo havitakuwa na maana kama yanayojadiliwa yanaachwa na wale wezi kiuendelea kula raha. Inasikitisha mno. COSOTA wao kushiriki kwenye kampeni za mtu mmoja kuna nini ndani yake?
 
Wasanii kuendelea kuibiwa wakati wao wapo inaonyesha wameshindwa kazi. Kuyasema haya ni lazima kwa faida ya kizazi cha sanaa. Kuna haja gani msanii kuimba pasi kupata chochote cha maana?
 
Kwanini maisha yake ya sanaa asiyatumie kwenye kilimo? Nadhani hili la kuvunjwa kwa mabaraza hayo na kupewa kazi watu wengi wengine kutachangia kwa kiasi kikubwa kuibua ari ya utendaji kwa wasanii na wasimamizi wao.
 
Ikumbukwe kwamba sanaa ni kazi na inaweza kuleta utajiri mkubwa kwa Taifa. Nchi za wenzetu wao wanafanikiwa kwa kupitia ulingo huo wa sanaa. Ndio, maana nasema katika majumuisho ya kikao hicho, ipo haja ya viongozi waliopo wa BASATA na ndugu zao COSOTA wawekwe pembeni kama wameshindwa wenyewe kuwajibika.
 
Huu sio wakati wa kuoneana haya. Tusimame kwenye ukweli na hapana shaka, Jenista Mhagama, mwenyekiti wa kamati hiyo ya Huduma za Jamii pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo watapata dawa hiyo kwa manufaa ya Taifa.
 
Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki wasanii wetu
 
0712 053949
0753 806087

Friday, October 21, 2011

Pigania ndoa yako mwanamama


NIANZE kwa kukushukuru wewe uliyepata nafasi ya kusoma kazi zangu, ikiwamo hii inayoelezea mambo ya uhusiano na maisha, yanayogusa hisia za wengi duniani.
Nasema hivyo maana suala la uhusiano ni zito kuliko inavyochukuliwa na baadhi ya watu. Baadhi yao wanafikiri kuwa wakiachana na waume zao leo, basi kesho atapata mwingine.



Sawa, ila sio jambo zuri. Sio njia nzuri katika maisha yako. Ni tabia mbaya inayotakiwa ipingwe na wote. Utajisikiaje ukiwa na umati wa watu ambao uliwahi kuwa na uhusiano nao?
Sio ajabu unaweza kuonekana wewe ni muhuni, maana kwanini uachwe na waume zaidi ya watano? Kwanini? Kuna nini hapo? Je, wewe ndio tatizo au mwenzako?
Haya ni maswali tunayotakiwa kujiuliza wote kwa pamoja ili kulinda ndoa zetu au uhusiano sisi wote. Msomaji wangu mpendwa, binadamu wengi tabia zao hufanana japo sio sana .
Japo kuwa kuna tabia mbaya na nzuri, ila mwisho wa siku, kwako wewe zinaweza kuwa kero. Hivyo, ukiona mwenzako anakwenda njia tofauti, unaweza kumuweka chini.
Lakini sio sababu ya kuvunja uhusiano wako haraka, maana umekutana na mtu njiani amekuvutia zaidi ya yule uliyekuwa naye. Ukifanya hivyo, ni kujiweka matatani.
Nasema hivyo maana unaweza kuondoka na kwenda kwa mwingine, ila ukakuta kasumba kubwa mno. Hapo hutafurahia zaidi ya kulia na kusaga meno. Ni baada ya kujidanganya mwenyewe.
Utashangaa kwanini ulifanya hivyo? Siku zote majuto ni mjukuu. Huna haja ya kulia. Ni wakati wako wa kuangalia mwenzako anakwendaje kwa kumuweka chini.
Ndio anaweza kuwa mnywaji sana wa pombe. Kwa bahati mbaya tabia yake ya ulevi wewe huitaki. Nadhani kwa kupitia wewe mwenyewe anaweza kuacha.
Ni baada ya kumwambia kistaarabu na kumuelezea jinsi gani anatakiwa awe ili aweze kuwa na wewe. Endapo yupo kwenye msingi wa kujenga nyumba yenu ya upendo anaweza kupunguza kama sio kuacha.
Nadhani hiyo ni tabia nzuri mno inayotakiwa ifanywe na wote, maana mapenzi mazuri siku zote ni kusikilizana. Hakuna njia ya mkato katika hilo . Ndio maana nasema pigania uhusiano wako.
Na kwa yule aliyejaliwa kufunga ndoa, basi ahakikishe kuwa analinda ndoa yake kwa kuzima zile dosari zinazoweza kuhatarisha usalama wa ndoa yake kwa sababu moja ama nyingine.
Wapo watu ambao kosa kidogo tayari wamedai talaka. Kwao wao ni bora wakimbilie talaka maana wameona mitaani wapo watu wanaoweza kuishi naye na kuendelea kujaza idadi ya wapenzi.
Inakera mno. Inatia aibu kama mtaa mzima umeumaliza kwa njia hiyo hiyo. Tabia ambazo baadhi yao zinaepukika endapo kwa mikono yako, mdomo wako na miguu yako itapigania kwa dhati suala hilo .
Watu watakucheka. Mwanamke kubadilisha wanaume zaidi ya watano kwa kipindi kifupi huo ni uhuni. Unajipakaza matope na kuonekana kituko mtaani na kuitwa majina mengi ya karaha.
Hutaweza kuwakataza watu kukuita wewe ni cha wote, jamvi la wageni na mengine lukuki. Kwanini uwakataze wakati ni kweli? Ajabu, utakapoitwa hivyo, watu watakusikia na kukuonea huruma.
Sio wote wanaweza kuwapenda wasichana wenye sifa mbaya kama hizo, hivyo ni wakati wako kujifunza kutokana na makosa. Muweke chini mtu wako kwa ajili yako.
Mfundishe tabia nzuri na upiganie kikweli uhusiano wako kwa faida yako na sio kukimbilia talaka au kuvunja mkataba wenu, maana sio vizuri na hakuna haja ya kujaza wanaume.

Thursday, October 20, 2011

Serikali ipige jicho lake BASATA

KUJADILI vitu vya maendeleo kwa Tanzania kunahitaji moyo wa chuma kama alivyowahi kusema muasisi wa Taifa hili, Hayati, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere juu ya masuala nyeti ya Azimio la Arusha.

                                                        Dayna Nyange, msanii

Mwalimu, mmoja wa viongozi wanaopendwa barani Afrika, Oktoba 14, ilikuwa ni kumbukumbu ya kifo chake, baada ya kumaliza siku zake za kuishi duniani, akitumika kama mkombozi kwa Taifa hili, linaloongozwa na Rais wake, Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Nasema moyo wa chuma, maana hata kama uwe mjuzi wa kujadili mambo hayo kwa kiasi gani, hao wanaojadiliwa kubadilika kwao ni kazi ngumu. Katu hawataki kusikia au kuona yale wanayofanya kwa faida ya nchi yao .
 
Hata hivyo, sio jambo la busara kubaki kimya. Taifa linazidi kutumbukia kwenye shimo baya la umasikini na wachache wao wakizidi kuneemeka. Utajiri ni wa kwao, wakati wenzao wanazidi kuwa masikini wa kutupwa.
 
Tanzania ya leo, ni kazi ngumu kupata ajira kama huna fedha. Suala kama hilo , linaonyesha ni jinsi gani mambo yanavyotakiwa kubadilika kwa faida ya wananchi wake. Tuache hayo turudi kwenye lengo la makala haya.
 
Wakati Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akiteua safu mpya ya uongozi ya baraza la Michezo Tanzania , nadhani ipo haja pia ya kuangalia upya mwenendo wa uongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
 
Baraza hili muhimu kwa Tanzania naweza kusema limekufa. Viongozi wake wengi hawaonyeshi jitihada zao za dhati kwa maendeleo ya sanaa ya Tanzania . Wasanii waliokuwapo bado kazi zao hazina jipya, huku wengineo tungo zao zikikosa sifa.
 
Ni hao wanaoacha kutunga nyimbo za kukosoa madawa ya kulevya, kubweteka majumbani au kwenye vijiwe vya kahawa, huzama zaidi kwenye tungo za kidunia. Hapa lazima niwe muwazi na bila ya kuweka woga wowote kwa ajili ya Tanzania .
 
Sitaki kusema viongozi wa BASATA wote wameshindwa kazi, ila Serikali lazima iwapige jicho ama kuwaelekeza vitu vizuri kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Nimepata nafasi ya kuchunguza utendaji kazi wa BASATA na kubaki mdomo wazi.
 
Mengi wanayofanya, si maendeleo kwa sanaa ya Tanzania . Uchunguzi wangu unaonyesha kila msanii wa nje anayekuja hapa nchini hutakiwa alipe fedha nyingi kama gharama za kuja kufanya kazi Tanzania , zisizopungua milioni moja.
 
Kwa mfano, wapo wanaotozwa hadi kiasi cha shilingi miliona moja, huku wakitakiwa walipe fedha za faini, kama mtu huyo ameanza kutoa habari kwa wanahabari kwa ajili ya kuwajulisha Watanzania.
 
Sawa, ila wakati mwingine wadau hao huonewa kwa makosa ambayo sio yao . Nasema hivyo huku nikiangalia upekuzi wa waandishi kujua habari hata zile wasizotakiwa wazifahamu kwa wakati huo.
 
Pamoja na hayo, kama ndivyo hivyo, fedha hizo za faini kiasi cha milioni moja hupelekwa wapi? Je, nchi hii inafanya juhudi gani kutangaza sanaa ya Tanzania ? Wasanii wetu wa ndani wanafanyiwa vitu gani kwa mafanikio yao ?
 
Msanii wa ndani kubaki kuimba peke yake ni jambo linaloweza kuangamiza kipaji chake. Inatakiwa apate ushindani, ama kusoma kutoka kwa wenzake. Hivyo basi, kitendo cha BASATA wao kujifanyia mambo kienyeji ni kuharibu mfumo mzima wa sanaa.
 
BASATA wao huku wakiweka mbele fedha, lazima utendaji kazi wao uwe mzuri, maana uliopo sasa ni kubuluzana na uliojaa maslahi binafsi. BASATA iliyopo sasa ni kuwakomoa wadau wenye uwezo wa kukuza sanaa kwa manufaa yao .
 
Sitaki nionekane tofauti juu ya hili, ndio maana hapo mwanzo wa makala haya nikatahadharisha maana wanaopewa ukweli hupayuka wakisema wanayojua wenyewe. Inatia aibu, kama kila mtu anahifanyia anavyojua mwenyewe.
 
Huku wadau tukipigania utendaji mbovu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), bado kuna vitengo nyeti vinaachwa tu bila kukosolewa. Nisema tu, nitakuwa mkweli kusema kila ninalojua kwa maendeleo ya Taifa langu, hata kama nitachukuliwa tofauti.
 
Kuna mambo mabaya mno yasiyofaa kufanywa na viongozi wetu, iwe ni kwenye michezo ama sanaa inayofaa kuheshimiwa Dunia nzima. Angalia Barani Ulaya, wengi wanafanikiwa. Muangalie mwanadada Rihannah, Jay Z na mke wake Beyonce, utakubali kuwa sanaa inalipa.
 
Sio huyo tu, bado wapo wakali wengine wanaovuna fedha lukuki, kutokana na kukuta mfumo mzuri katika nchi zao, ikiwamo hakimiliki. Siamini kama wasanii wetu wa ndani wataendelea kuachwa tu, hali ya kuwa wana utajiri wa vipaji.
 
Ni wakati wao Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuangalia upya sera zao na sera za mabaraza yake, likiwamo hilo la BASATA. Sioni juhudi na harakati za kukuza sanaa ya Tanzania zaidi ya kuidumaza.
 
Je, ni wasanii wote wanatakiwa walipe fedha hizo zikiwamo faini au ni wachache? Ushahidi unaonyesha kuwa, kama ni kweli, basi BASATA wanavuna fedha nyingi, maana wengi wanakiuka masharti hayo. Yani kupata kibali, kabla ya kuvuja kwa ujio wao.
 
Hivi kweli, mwandishi kuandika ujio wa msanii fulani ni kitendo kibaya kiasi cha kuwafanya BASATA walazimike kutoza faini hizo? Jamani, kwanini Tanzania tunakwenda ovyo namna hiyo?
 
Kwanini tamaa ya kujaza matumbo yetu ipo mbele kuliko kusudio la kweli la kuwakomboa Watanzania kwenye vita hii ngumu ya maradhi, ujinga na umasikini? Sikatai, msanii alipe gharama za kuishi nchini, ila nyingine ni wizi tu.
 
BASATA unaweza kufuatilia kibali kwa muda mrefu bila hata kukupatia. Nia yao ni mdau huyo avunje amri yao ya kuzungumzia ujio huo hata kwa marafiki zake, ili wapate hiyo shilingi laki tano au milioni moja.
 
Yuko wapi Emmanuel Nchimbi, waziri wa Wizara hiyo? Hivi kweli ndivyo BASATA wanavyotakiwa wajiendeshe? Sina nia mbaya, ila kusudio ni kujiendesha vema kwa manufaa ya Tanzania na sio kwenda ndivyo sivyo.
 
BASATA wanatakiwa wasome alama za nyakati. Wanatakiwa wawe na fikra pevu juu ya sanaa ya Tanzania , inayozidi kuyumba. Wengi kazi zao ni mbaya na zinakosa maudhui na maana halisi ya sanaa ya Tanzania , hata kwenye matamshi.
 
Bado sanaa nyingine zinakosa mwamko, ikiwamo ya nyimbo za asili, zile za makabila tofauti, zilizokuwa zikivuma wakati huo. Sanaa kama ususi, uchongaji, uchoraji sasa zimeadimika kabisa katika Taifa hili.
 
Wanaotamba ni Bongo Fleva, tena kwa kazi ambazo nyepesi, zimekosa soko na mvuto linapokuja soko la Kimataifa. Wengi wao mavazi yao ni karaha tupu. Bado wabunifu ni mavazi wapo wapo tu. Ukienda nchi za wenzetu wamefanikiwa, kiasi cha sasa kuangalia mazuri yao .
 
Sisi tuna wasanii wengi tu, lakini bado Makhirikhiri wamekuja kuteka soko la Tanzania, bila kusahau ndugu zao Dikakapa Traditional Dance, ambao hadi sasa wapo mikoani huko wakitangaza muziki wao wa asili.
 
Sawa, waje tu, maana najua ni somo kwa wadau, viongozi na wasanii wa ndani. Lakini kuwekewa ngumu, au wadau kutozwa fedha nyingi ni kuwadhulumu wao na kuibananga sanaa ya Tanzania , inayotakiwa itangazwe na kila mmoja wetu.
 
Kiu yangu ni kuona sanaa inapiga hatua kwa kuwa na viongozi wenye uelewa, mipango na uthubutu katika kazi zao, sio wale wanaotamani zaidi kumiliki vitu vya thamani katika utawala wao, huku wanavyoviongoza vikijikongoja.
 
Ndio maana naitaka Serikali, kuangalia zaidi mfumo mzima wa BASATA na ndugu zao COSOTA, maana ni muhimu na wameshika funguo za mafanikio kisanaa ya wasanii wa Tanzania , wanaoshi kama njiwa, kula chini kulala juu.
 
Naomba kutoa hoja waungwana
0712 053949
0753 806087

Friday, October 14, 2011

TFF rekebisheni mwenendo wenu



WAKATI mwingine kusema ukweli ni jambo jema japokuwa hao wanaosemwa au kupewa ushauri huo, watajisikia tofauti kwa namna moja ama nyingine.

Inawezekana sisi ni watu wa karibu kabisa katika ufanyaji kazi huo, ila linapokuja suala la ukweli hakuna jinsi. Tuambiane tu kwa nia ya kufika pale tunapohitaji.

Jamani, kwenye ukweli siku uongo hujitenga. Hivyo hakuna haja ya kuogopana. Ni kutokana na hilo, acha niseme kuwa Shirikisho la Soka nchini (TFF), chini ya Rais wake, Leodgar Tenga, tujiandaye kulia zaidi.

Katu tusijidanganye kupiga hatua kamwe. Wala tusitarajie kupanda viwango vya soka vya juu zaidi au kucheza michuano mikubwa duniani, ikiwamo Kombe la Dunia.

Tunachotakiwa sisi ni kujiandaa kulia zaidi kwa kuporomoka kwenye michezo, maana viongozi wengi wanafanya kazi zao kisiasa zaidi wakiwa na nia ya kulindana hata pale watu hao wanapoharibu na kuwakera watu.

Nikiwa kama mdau wa michezo, nitamlaumu Tenga kwakuwa ndiyo Rais, ila zaidi wa kubeba lawama hizo ni Katibu Mkuu wake, Angetile Osiah.



 Tenga kulia na Sunday Kayuni
Ndio, maana yeye ndio mtendaji mkuu wa yote japo kuwa amekuwa mwepesi mno kujitetea au kumtetea yule anayeonekana tofauti kwenye utendaji kazi wake.

Angalia mwenendo wa timu ya taifa, Taifa Stars. Ni utumbo mtupu. Kila mara kumekuwa na kasumba za hapa na pale. Klabu zinakwenda ndivyo sivyo.

Osiah bila kujua analofanya, anajichanganya zaidi kwa kumuondolea majukumu yake, Mkurugenzi wa Ufundi, Sunday Kayuni. Eti kuboronga kote huko hakusababishwi na yeye, wakati anajua fika ufundi wote upo chini yake.

Kwa madai yake, wa kulaumiwa ni watu wengine wakiwamo wakuu wa mashindano. Jamani, kabla ya kufika huko kwenye mashindano, lazima ufundi utangulie.

Ni yeye wa kuangalia ratiba zinakwendaje ili mambo yaende vizuri. Kubadilishwa ovyo kwa mechi za ligi kuu au vitu kuingiliana kumesababishwa nay eye.

Wala sina haja ya kutoana kafara hapa, kama walivyomtoa kafara Ofisa Habari wao wa zamani, Florian Kaiajage kwenye tukio la kugoma CD ya wimbo wa Taifa, ila ukweli lazima usemwe maana baadhi ya Watanzania, hawajui wajibu wao.

Hakuna mipango kabisa TFF. Hawasimamii michakato ya kupiga hatua katika sekta ya michezo, ukiwamo mpira wa miguu, zaidi ya kukalia vyeo wasivyoviweza.

Kwa bahati mbaya au nzuri, wanaojitolea kusema ukweli huonekana tofauti katika nyuso zao na kusemwa kupita kiasi, wakijifanya wao ni miungu watu wasioweza kukosea.

Eti, ndio tatizo na watapekelekea wadhamini wawatose kwa namna moja ama nyingine. Jamani, hakuna malaika hapo. Hakuna aliyekamilika. Kukoselewa kuna maana ya kujipanga ili Taifa lipige hatua kutoka hapa lilipo.

TFF wamekosa changamoto na ari kwa wadau na wachezaji wote, kuanzia Taifa Stars na wale wanaocheza ligi. Ndio maana ligi inakosa mvuto kwa ratiba mbovu.

Mara kadhaa timu ya taifa, Taifa Stars, inakosa mechi za kujipima nguvu, kitu kinachoifanya ishindwe kupiga hatua kutokana na maandalizi yao hafifu.

Ni matatizo makubwa. Kwa timu kama hiyo isiyokuwa na jipya, inahitaji maandalizi ya uhakika na wala sio kuzima moto kama wanavyofanya sasa na kufuja fedha za walalahoi.

Ona, hawa wameanza kulinganisha uwepo wa Osiah na ule wa Fredrick Mwakalebela. Mwakalebela ni Katibu Mkuu wa zamani, aliyemaliza muda wake na kuhamia kwenye siasa.

Huko alishindwa kuingia bungeni kwa sababu anazojua mwenyewe na chama chake. Sitaki kuingia huko kwenye siasa, maana ndizo zinazoharibu mfumo wetu wa maendeleo ya michezo.

Wakati wa Mwakalebela, hakujatokea hayo yanayotokea sasa. Na hata kama yaliyotokea, basi si kwa kiwango kikubwa kama inavyokuwa sasa kiasi cha kukosa kusafiri kwa timu ya Taifa, huku klabu ikifanikiwa kwenda Sudan.

wachezaji wa Tanzania wanayecheza soka la kulipwa nje walikuwa wakiwasili kwa wakati tofauti na sasa. Hakuna mawasiliano mazuri wao na Mashirikisho mengine duniani.

Kulikuwa na mawasiliano ya uhakika. Mechi za kujipima nguvu zilikuwa za kutosha. Hali hiyo ilimfanya hata kocha wa wakati huo, Mbrazil, Marcio Maximo, afanye kazi yake vizuri.

Leo hii baadhi ya wadau wameanza kumtupia lawama kocha wa sasa wa Stars, Mdenmark, Jan Borge Poulsen. Hoja wanayo, ila pia wasisahu na ubabaishaji huu wa TFF.

Nadhani wanafanya hivyo kwasababu kocha ndiyo mwenye jukumu hilo, lakini wakati mwingine tunaweza kumuonea na kumtupia mzigo wa bure, wakati anashindwa kusimamiwa na viongozi hao wa TFF wanaojaribu kukwepa majukumu yao.

Hasaidiwi huyu. Hata akisaidiwa, wakubwa hao huangalia namna ya kupambana na wezi wa milangoni na kusahau mengine, maana nia yao ni kuingiza mapato ya kutosha.

Kwanini viongozi wasikubali kushindwa na kuweka mipango mingine? Hatuna ligi nzuri yenye ushindani.

Hatuna msingi imara wa kuendeleza vijana wadogo, bado tunaota ndoto ya kuwa na kiwango imara. TFF wa leo, wakiulizwa vijana wanaopatikana kwenye michuano ya Copa Coca-cola leo wanafanya nini hawatakuwa na jibu hilo.

Uwapi umuhimu wa kuwa na ligi hiyo? Huko wilayani kwenye vijana wengi kuna endelea na nini? Mkurugenzi wa Ufundi, Kayuni kazi zake ni zipi pale TFF?

Ziwekwe wazi ili wadau wazijuwe. Ni hapo ndipo ninapojikuta nikishindwa kuwaelewa TFF.

Najua ni kazi ngumu kusema ukweli, ila kwa hali ilivyo, Watanzania wajiandaye kulia zaidi, maana mafanikio kwetu ni ngumu na tusijidanganyane kwa hilo.

Hatuwezi kufanikiwa wakati tunafanya kazi midomoni. Ni ngumu kupiga hatua wakati sisi tunachojua ni kusawazisha kauli zinazopingwa na wadau, ili waonekane viongozi wazuri kwa jamii wakati ni uongo mtupu.

Osiah ambaye ndio mtendaji mkuu wa TFF, kazi yake imekuwa ngumu mno. Ameshindwa kuwa na ushawishi kwa wadau na upo uwezekano wa kuwapoteza hata wadhamini waliokuwapo sasa kwenye timu zetu.

Najua Osiah ni ndugu yetu ila kumuangalia anavyokwenda ni kumuharibia. Watu wanamuona. Sifa yake inazidi kupotea kwa ubabaishaji wake.

Binafsi napenda kuona anakwenda vizuri na ndio maana nakuwa muwazi kwa ufanyaji wake wa kazi. Hana jipya. Ajaribu kuangalia namna anavyoweza kujiendesha.

Kama ni mpole awe mkali zaidi. Zipo tetesi zinazodai kuwa Osiah licha ya kuwa na cheo hicho, lakini wapo watu wa chini yake wanamuendesha.

Sitaki kuliamini hilo japokuwa najua lisemwalo lipo, maana nia ni kuwekana sawa ili Tanzania ipige hatua katika sekta ya michezo, ukiwamo huo mpira wa miguu.

Kwanini? Hivi kweli sisi tunakuwa watu wa kuchekelea mafanikio ya wenzetu, wakati tuna idadi kubwa ya wanamichezo waliozagaa katika wilaya mbambali.

Fanya uchunguzi utakubaliana na mimi. Huko Handeni mkoani Tanga, Iringa, Mtwara, Tarime, Morogoro na kwengineko kumejaa vipaji vya hali ya juu ila hawaendelezwi wala hawaibuliwi kutokana na mipango yenye tija na Tanzania.

Vijana hao wanakosa walau jezi za kuvaa wakati tuna TFF inayoungwa mkono na wadau wakubwa tu. Sitaki kuamini kama muda umekwisha, maana wanaweza kujirekebisha na kusonga mbele wakiacha kasumba zao.

Kwa sasa TFF hawana jipya. Viongozi wapo wapo tu kwenye viti vyao vya kuzuunguka. Kusua sua huku kukiendelea, lawama hizi ni zenu, maana wadau wanawaunga mkono.

Tatizo lipo wapi?  Siasa? Ubinafsi ama ni kuogopana? Kila mtu lazima afanye kazi yake kama inavyotakiwa. Tenga, lazima awe mkali kwa vijana wake ili mambo yaende.

Osiah lazima akubali kukosolewa na watu wakiwamo wanahabari ambao kifani ni ndugu zake kabisa. Naye ni mwanahabari hivyo uwepo wake TFF ni mafanikio kwa waandishi wote nchini wakiona mwenzao anakwenda vema.

Malalamiko mengi yamekuwa kwa vyama vingine vya michezo miaka nenda rudi maana ufanyaji kazi wao ni wa midomoni.

Faida yao wanaijua, ndio maana kila siku malalamiko yao ni fedha za maandalizi na hakuna anaewasikiliza.

Wakati huo TFF wao walitulia lakini kwa bahati mbaya sasa kibao kinaanza kuwaugeukia wao. Zindukeni nyie? Kumbushaneni wajibu wenu. Punda hawezi kwenda bila mchapo.

Binafsi nipo tayari kwa lawama maana najua siku zote sio mzigo ili mradi ujumbe wangu umewafikia.

Kwa mwendo huu wa TFF, kikweli maendeleo ya soka ni ndoto ya kuku kutamani kunyonyesha watoto wake.

Naomba kutoa hoja waungwana.

0712 053949
0753 806087

Saturday, October 01, 2011

Meneja wa Sinta amwaga sera


MENEJA wa msanii wa filamu aliyewahi kutamba mno miaka ya nyuma, Christina Manongi, Richard Methew, amesema filamu itakayowakutanisha mwanadada huyo na Juma Kassim maarufu kama ‘Juma Nature’, itakuwa moto wa kuotea mbali, endapo makubaliano yao yatafikiwa na wawili hao.

Kwa siku kadhaa sasa wawili hao wamekuwa wakikutanishwa kwa nia ya kupatanishwa ili wacheze filamu hiyo, baada ya kuingia kwenye malumbano, yaliyosababisha Juma Nature atunge vibao viwili vya ‘Sitaki Demu’ na ‘Inaniuma Sana’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Methew alisema hadi sasa Sinta bado hajakuwa tayari, licha ya kuonekana kuelekea kwenye makubaliano hayo.

Alisema mara baada ya kufikia makubaliano yao, wawili hao watacheza filamu hiyo na kutangazwa kwa wadau kwa nia ya kuona kazi yao inakuwa nzuri.

“Nimejaribu kuangalia vipi Sinta anaweza kurudi kwenye sanaa yake, huku nikiamini kuwa akicheza na Nature inaweza kuwa kazi nzuri zaidi na kumrudisha kileleni.

“Najivunia kuwa na msanii kama Sinta, hivyo naamini akifikia makubaliano kwa kusahau yote yaliyopita, mambo yanaweza kuwa mazuri zaidi,” alisema Mathew.

Hata hivyo, Sinta alipozungumza na Gazeti hili jana, alisema hana nia ya kurudi kwenye uhusiano wa kimapenzi na Juma Nature, hivyo wadau wanapaswa kuelewa katika hilo.



                                 Juma Nature chini na Sinta juu.  
Mwanadada huyo ni miongoni mwa wasanii wa kike mahiri na wanaosubiriwa kwa hamu kubwa katika ulingo wa filamu, huku umbo na sura yake likichanganya wengi, tangu wakati huo anashiriki katika michezo ya kundi la Kaole Sanaa Group.

Kago kwaheri Simba


WAKATI klabu ya Simba, ikitarajiwa kuanza mazoezi leo kwa ajili ya kujiandaa zaidi na mechi za ligi kuu, mshambuliaji wa Kimataifa, Gervas Kago, ameombwa na nchi yake kwenda kujiunga na timu yake ya Taifa.

Hiyo ni baada ya Afrika ya Kati, kuwasilisha barua yao jana, wakati tayari alishajua kuwa ataanza mazoezi na wenzake, licha ya nyota wanne wa Simba, kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars, kinachonolewa na Mdenmark, Jan Poulsen.

Wachezaji hao wa Simba walioingia kambini wakijiandaa na safari yao ya Morocco, ni Juma Kaseja, Juma Nyoso, Victor Costa na Amir Mafta.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, alisema kuwa kupokea barua hiyo kunaonyesha kuwa naye hatajiunga na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na patashika ya ligi ya Vodacom.

Simba wanaendelea na mikakati yao wakati Yanga wao wamesimama mazoezi kwa ajili ya kupisha maandalizi ya Stars, kitu kilichomfanya kocha wao, Mganda, Sam Timbe, kurudi kwao kwa muda.

                               Gervas Kago
“Tunashughulikia usafiri wao kuanzia sasa, nadhani naye hatakuwapo kwenye timu yetu kwa ajili ya kuwakilisha Taifa lake, Afrika ya Kati.

“Ni jambo zuri mchezaji kuwamo kwenye kikosi cha timu ya Taifa, hivyo wale wote ambao hawapo kwenye timu zao za Taifa, kesho (leo) wataanza mazoezi,” alisema Kamwaga.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 18, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 15, wakati Yanga wao wana pointi 12, wakizinduka katika mechi mbili zilizopita na kuonyesha kiu ya kutaka kutetea ubingwa wao huo.

Friday, September 30, 2011

Wakali wa Ulaya walivyotoana jasho







MICHUANO ya klabu Bingwa Ulaya iliendelea tena Jumanne na Jumatano katika viwanja mbalimbali barani Ulaya.

Katika mechi za Jumanne Manchester United ikiwa nyumbani ilitoka sare ya mabao 3-3 na Basel FC ya Uswisi.
Dany Welbeck alipachika mabao mawili ya haraka dakika ya 16 na 16……………., lakini Fabian Frei alifunga bao kipindi cha pili kabla ya kaka yake, Alexander Frei akufunga mengine mawili na kuwaweka mbele, lakini Ashelay Young alisawazishia United.

Mechi nyingine ilikuwa ni kati ya Bayern Munich dhidi ya Man City katika Uwanja wa Allianz Arena, ambapo mabao mawili ya Mario Gomez yaliilaza City.
Trabzonspor walitoka sare ya bao 1 – 1na  Lille, Real Madrid wakiwa nyumbani waliichapa Ajax mabao 3 – 0 yakifungwa na Ronaldo, Kaka na Karim Benzema.

Otelul Galati wa walifungwa na Benfica nyumbani bao 0-1,  Napoli          waliishinda mabao 2 – 0 dhidi ya Villarreal,
Lyon wakaibanjua 2 - 0 Dinamo Zagreb na Inter Milan waliifunga CSKA Moscow 2 – 3.

Kwenye mechi za Jumatano Chelsea walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Valencia, bao la Chelsea lilkuwa la kwanza likifungwa na Frank Lampard kabla ya  Soldado kusawazisha kwa penalty.
Arsenal ambao msimu huu wamekuwa hawapewi nafasi kubwa kutokana na kuanza vibaya kwenye Ligi ya England, wameichapa Olympiacos mabao 2-1, bao la kwanza lilifungwa na Alex  Oxlade-Chamberlain dakika ya 7 na la pili lilipatikana dakika ya …………………………….. Andre Santos (19),  David Fuster aliipatia timu yake bao la kufutia machozi dakika ya 26.

Shakhtar Donetsk walitoka sare na 1 – 1 Apoel Nicosia, Marseille          waliichapa mabao 3 - 0   Borussia Dortmund, Bayer Leverkusen ilishinda 2 – 0 dhidi ya Genk na Zenit St Petersburg waliizamisha FC Porto mabao3 – 1.

BATE walikula kichapa cha mabao 5 –0 kutoka kwa Barcelona, mchezaji wa BATE alianza kujifunga dakika za mwanzo, Messi aliweka nyavuni mara mbili, Pedro na Villa kila mmoja akifunga moja.
AC Milan waliifunga 2 - 0    Plzen, Ibrahimovic na Cassano waliipatia ushindi huo klabu hiyo yenye makazi yake San Siro.

Sumalee mdheee wa Hakunagaaa


HAKUNAAGA zaidi yangu mi na wewe, hakunaaga zaidi yangu mi na wewe, hakunaaga zaidi yangu mi na wewe, hakunaaga zaidi yangu mi na wewe, hakunaaa, hakunaga, hakunaaa hakunaga.
Hiko ni kiitikio cha wimbo mpya wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Suma Lee, uitwao Hakunaga, kibao ambacho kimepigwa katika mahadhi ya kwaito.
Wimbo huo tayari umeanza kuwabamba mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva na kupata Air Time katika vituo mbalimbali vya redio, huku video ya wimbo huo ukifanya vizuri pia.



Sumalee akiwa katika picha tofauti...
Sasa mkali huyo anatamba na wimbo wake wa 'Hakunaga'
Msanii huyo alianza masuala ya muziki kwa mara ya kwanza mwaka 2000 na moja kwa moja akaingia studio na kutoa wimbo ulioitwa Sivuti na Mama, akiwa na kundi la Parklane lililokuwa na makazi yake mjini Tanga.
Hakuweza kufanya muziki kabla ya hapo kwa kuwa familia yake haikuwa tayari kumuacha ajiingize katika masuala hayo, lakini muda ulipofika yeye mwenyewe aliamua liwalo na liwe.
Ingawa hakuwahi kufanya muziki kabla ya hapo, lakini aliweza kuingia studio, ambapo mwaka huo waliweza kutoa wimbo mwingine uitwao Aisha, wakati huo C Pwaa alikuwa amejiunga na kundi hilo la Parklane.



Baada ya Parklane kusambaratika, wasanii waliounda kundi hilo kila mmoja alijishughulisha na muziki binafsi.
Suma Lee, ambaye jina lake halisi ni Ismail Thabit, aliyezaliwa Tanga katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo, mwaka 2006 alitoka kivyake na kibao kiitwacho Chungwa.
Wimbo huo uliweza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio, huku ikishika katika chati za vituo hivyo vya redio hapa nchini na nje ya mipaka yetu.
Suma alitoa albamu ambapo wimbo huo wa Chungwa ndio ulibeba jina la albamu, zikiwemo nyimbo nyingine kama Rafiki, Chaguo Lake, Gomba na Ba na Ma.
Kutoka kwa kibao cha Hakunaga ni maandalizi ya albamu yake mpya baada ya ile ya kwanza ya Chungwa.
Albamu hiyo mpya itakayoitwa Hesabu za Mapenzi itakuwa na nyimbo 15, ukiwemo wimbo mkali uliofanya vizuri mwaka 2009 uitwao Ndani One Week.
Katika albamu hiyo mpya kutakuwa na nyimbo kama
Nikueleze, Uk Dubai, Aunt na Hakunaga pamoja na Ndani One Week ambazo tayari ameshaziachia.
Suma Lee amekuwa na utaratibu wa aina ya pekee tofauti na wasanii wengine, kwani huchukua muda mrefu hadi kutoa ‘single’ moja hadi nyingine.
Singo ya mwisho Suma Lee kutoa ilikuwa ni Ndani ya One Week, ambayo ilikuwa mwaka 2009 na kufanya vizuri, hivyo ni takribani miaka miwili imepita ndio ametoa Hakunaga.
Akitoa sababu za kuchelewa kutoa singo baada ya kutoa moja, amesema huo ni utaratibu wake, kwani akifanya haraka mashabiki wake watamchoka kama wanavyochokwa wengine.
“Wimbo wangu mmoja ukiusikiliza leo, ndivyo utakuwa na utamu ule ule utakapousikia tena baada ya miaka 10 kupita,” anasema nyota huyo.
Tangu msanii huyo aanze muziki kwa mara ya kwanza mwaka 2000 hadi leo 2011 ni miaka 10 imepita, lakini bado ameonyesha uwezo aliokuwa nao zamani.
Ni miaka 10 sasa tangu aanze sanaa, lakini bado uwezo wake wa kutunga mashairi na kuimba ni wa kipekee na ndiyo maana anaweza akakaa miaka miwili bila ya kutoa wimbo na akija kutoa unakuwa mkali.
Kwa sasa Suma Lee ana mpango wa kutafuta vijana wenye sauti za ukweli na wenye uwezo wa kuimba na kuweza kuinua vipaji vyao.
‘Project’ hiyo ya kuibua vipaji na kuviendeleza ameipa jina la Voice of Suma, ikilenga wale wasanii wadogo wenye sauti nzuri na uwezo wa kuimba kama yeye.

Mjuwe Marlaw kifaa cha Besta





Marlaw akiwa na Bestaaaa


BABA mwimbaji, mama mwimbaji – tazama familia hii, kama atapatikana mtoto itakuwaje?
Swali kama hilo pia unaweza kujiuliza kuhusu Beyonce Knowles na mumewe Shawn Carter ‘Jay-Z’.
Lakini, katika jukwaa la muziki wa Tanzania, hasa wa kizazi kipya, naizungumzia familia iliyoanzishwa na Marima Lawrence na Besta Rugeiyamu.
Wawili hao ni wanandoa na pia ni waimbaji mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, wakati mume akijulikana vyema na mashabiki wake kama Marlaw na mke akitambulika kwa jina la Besta.
Unadhani akipatikana mtoto kwenye familia hiyo atarithi kitu gani? Kwa haraka utasema ni muziki, na kuzitazama kama familia ya Will Smith na mkewe Jada Pinkett – ambao watoto wao, Jayden na Willow, wanatesa kwenye muziki na filamu kama ilivyo kwa wazazi wao.
Mkali huyo alitupasha kuwa yote juu ya ndoa yake na masuala mazima ya muziki.
Tanzania inamtambua Marlaw kutokana na kujishirikisha na sanaa ya muziki, lakini malengo ya mwimbaji huyo ni kuufikisha mbali muziki wake, ikiwa pamoja na kutambulika katika bara zima la Afrika.
Wakati akiwa na fikira hizo, Marlaw anatambua ujio wa waimbaji wapya ambao wanaongeza ushindani katika tasnia hiyo hapa nchini.
“Kuongezeka kwa wasanii kunazidisha ushindani na kuibua changamoto mpya katika muziki,” anasema.
Muziki umekuwa ni sehemu ya maisha kwa msanii huyo, tofauti na ilivyokua mwanzo wakati anaanza kufanya kazi hiyo.
Marlaw, ambaye alikuwa msanii kutoka Tanzania House Of Talent (THT), alijiunga katika jumba hilo la vipaji kwa ajili ya kujiongeza ujuzi zaidi baada ya kuachia kibao chake cha Bembeleza mwaka 2007.
Marlaw alijifunza mambo mengi THT, ukiachilia uimbaji, pia aliweza kujifunza namna ya ‘kuperform’  na bendi ‘live’.
Baada ya kuachia Bembeleza, msanii huyu alikaa kimya kwa muda akijipanga upya na kuachia nyimbo nyingine kibao kama Rita, Daima na Milele, Bado Umenuna aliyomshirikisha Chid Benzi na Pii Pii (Missing my Baby).
Marlaw anatamba katika soko la muziki na albamu zake mbili ya kwanza ikiwa ni Bembeleza na ya pili ni Bidii.
Albamu ya Bembeleza iliitoa Septemba (2007) ikiwa na nyimbo (12), ambazo ni Bembeleza, Rita, Bado Umenuna, Daima na Milele, Busu la Pink, Si mimi.
Wakati ile ya Bidii iliyoitoa Septemba (2009) ilikuwa na nyimbo 12 pia,  zikiwemo Pii Pii (Missing my Baby), Sorry Sana, Be Happy na Tanzania.
 Msanii huyo alikutana na mkewe, Besta kwenye muziki wakawa na uhusiano, huku wakiendelea na tasnia hiyo hadi walipoamua kufunga ndoa ili kuwa mke na mume.
Akizungumzia juu Serikali kusaidia sanaa hiyo ya muziki, Marlaw anasema kuwa iko tayari kusaidia na ndio maana imeanza na msaada wa studio ya ‘mastering’, kitu ambacho ni muhimu sana kwa kazi zetu.
Pia alizungumzia muziki wa nje na ule wa kwetu akisema muziki wa nje una maendeleo mazuri, kwa kuwa wana mifumo madhubuti kwenye pande zote za haki ya sanaa kuanzia usambazaji wa kazi, haki miliki na hata matumizi ya sanaa kiujumla.
Kwa sasa unapomzungumzia Marlaw ni kama unauzunguzia muziki, kwa sababu chakula chake anakipata kutokana na kufanya muziki, makazi yake anayolala yanatokana na ujira anaopata kwenye muziki, lakini kubwa kwenye mapenzi – mkewe ni mwimbaji.


Sinta kubali mama weeee, ehee





 Sinta akiwa katika pozi bomba mbayaaaaaaaaaa. Huyu kweli ni malkia na anastahili kuitwa mrembo.
Chini ni ujumbe wake mzito kwa mashabiki wake wooote kwenye mtandao wa facebook na yaliyofuata ni maoni na ushauri wa marafiki zake haooo.

Kikweli handenikwetu.blogsport.com inatamani kuona wawili hao wanacheza movie hiyo ambayo kwa mujibu wa meneja wa Sinta, Richard Mathew, wawili hao wanaelekea makubaliano.

Christine Sintah
hi Sintah's fans,baada ya miaka 9 siongei na hatupikiki chungu kimoja na Nature unafikiri, ninaweza kusamehe yaliyotokea na kufanya nae kazi ya movie na ikaenda platinum?pse comment KISTAARABU
LikeUnlike · · Wednesday at 7:41am via BlackBerry · Privacy:Shared with: Christine's friends

     
            Emilian Lyimo samehe mtoto mbona hata mm ulinisamehe tupilia mbali issue tofauti
            Wednesday at 9:17am · LikeUnlike
            Mary Misoji Ng'oboko Kusamehe ni muhimu mamy katika maisha maana kwanza utakua umeutua mzigo fulani mkubwa moyoni... hata maandiko ya mungu yanatusisitiza msamaha....Kama ni kazi tu fanyeni ila ule ukaribu kama zamani usiwepo... ukaribu wenu ni wakati wa kazi t

            Wednesday at 9:17am · LikeUnlike
            Martin Josephat Kwanza mtakapo fanikiwa ukiigiza hiyo Movie mtakuwa mmewasaidia wale wote ambao wanavibifu visivyo na maana na kujiona wanachofanya ni ujinga tu na mwisho wa siku wenda mambo kama hayo yakapungua na kama si kuisha kaisa!
            Wednesday at 9:21am · LikeUnlike · 1 personLoading...

            Fadhil Ally
            SINTAH samehe kama binadam na sio sababu ya mapenzi au kazi coz kama mapenzi yalishakufa na kama makosa wote mlifanya n kumbuka NATURE ni celebrity than you, so swala kusameheana ni swala la kibinadam na sio u celebrity, mapenzi au ela, bad...o ujamaliza maisha u never know what wil happen 2mr...... Sisi wazawa wa TEMEKE atuna kinyogo coz tupo fasta kusahau na kusamehe, so NAAMINI nature ashasamehe yupo busy na kazi zake kama ulivyo wewe, achana na washamba wa maisha wanaokupa mawazo ya kitoto waambie sijui nini kesho kitatokea mbele then watajua binadam ni nani,See More
            Wednesday at 9:21am · LikeUnlike

            Verdiana Mathias Mimi nafikiri msamaha wa kwl unatoka ndani ya nafsi ya m2,haitaji mawazo ya wa2 wa pembeni,jee km wa2 wote wakisema ucmsamehe so hutomsamehe?lbd uliza km jee ufanye nae kazi,lkn dini ye2 inasema samehe 7mara70 hamna mkamilifu duniani
            Wednesday at 9:22am · LikeUnlike

            Nelson Karabwe Mie nadhani hilo niwazo zuri sana Sinta.Kweli kusamehe ni jambo muhim sana kusamehe jambo jema Sinta,MPE ISSUE BRO.Wala sikosa kuuliza wadau kwani humu ndani sio tangazo kama gazetini.
            Wednesday at 9:23am · LikeUnlike

            Idd Minani Hey sinta forgive and forget there u will release ur self from anger and strases dont try to rise the dead u have to let it go
            Wednesday at 9:29am · LikeUnlike

            Olivia Sanare-mwanaharakati Hehehehehe siku ya kwanza kukutana nae alikuja kwetu usikuuu,HAKUNA KUMSAMEHE ANATAFUTA PAKUANDIKIA MISTARI MINGINE TWIN HANA NYIMBO CKU HIZI.
            Wednesday at 9:31am · LikeUnlike · 1 personLoading...

            Sarah Albert Sintah dear samehe ufanye kazi, yaliyopita c ndwele mama
            Wednesday at 9:34am · LikeUnlike

            Bobson'dozen Julius itapendeza sana coz mlikua mnapendezana sana akuna mahusiano yaliyotokea kupendwa kama yenu coz yalikua ya kwanza ya msanii kudat na msanii
            Wednesday at 9:36am · LikeUnlike
 

         Kaka Ommy kama kuna aliekushauri juu ya hili mpe pongezi sana na kama ni akili zako ongera nyingi,ilo ni la kulifanyia kazi mazima sio mda wa mabiifu huu ni amani na kusaka hela tu
            Wednesday at 9:40am · LikeUnlike · 2 peopleLoading...

            Vicent Mgunda Igosha Huwezi jua kesho wenda akaoa mtoto wako samehe tu ilikuwa utoto sintah
            Wednesday at 9:47am · LikeUnlike

            Okot P'Bitek iTAKUWA POA SANA CAUSE KILA M2 ATAMUHESHIM MWENZIE SAHAU FANYA KAZ YALIYOPITA YAMEPITA!
            Wednesday at 9:52am · LikeUnlike

            Aysha Nyange Kiukwe sintah mi cdhani km cns dat tym mpk leo huongei nae kunachochote kimekuathir au laah' bc jua ht ukimsamehe it will b da same nothing change.. Ckiliza moyo wako zn fanya maamuz my dia.. Wt evr ur decition is' it will b u mamaa....
            Wednesday at 9:56am · LikeUnlike

            Bakari Hemed km uwez kusamehe itakua ngumu kupata msamaa, jifunze kupitisha msamaa km maji kwenye mto.
            Wednesday at 10:15am · LikeUnlike

            Faraji Said Kemea pepo lakinyongo linalokusumbua.
            Wednesday at 10:16am · LikeUnlike

            Chris Kaoneka Mjomba Oliver Nakumbuka the First time huo wimbo unapigwa Nilikuwa na Mjomba Tina kwenye Gari alilia sana...! Venture alimtumia sms akamwambia kuna wimbo sikiliza...! Umenikumbusha Mbali sana...! Hahaha...! Tinah Samehe tu Mjomba...! Yameisha fanya kazi iwe tu ina hela ndefu...!
            Wednesday at 10:20am · LikeUnlike

            Samson Simbeye jaman kuna gazeti1 la udaku limetoka leo lasema kwamba hao watu now wapo pamoja na tofauti zao zimeshaisha so tueleweje?
            Wednesday at 10:25am · LikeUnlike

            Saida Salum My dear just follow your heart.
            Wednesday at 10:28am · LikeUnlike

            Ezekiel Noah Leo tumia status hii kujua maadui zako na ambao hawakutakii mema,utaona wanafiki wote wasiokupenda watakwambia usimsamehe na kukumbushia machungu achana nao kwani hata huku kwetu wapo wapotezee. samehe fanya kazi na Kibra itakujengea heshima na utaonekana umekomaa!hebu angalia comment za fans wengi wanapenda umsamehe nina imani utafanya hivyo.
            Wednesday at 10:31am · LikeUnlike

            Jacqueline Mwibule samehe my dia km Mungu husamehe kwanini wewe????wala hakukupunguzii kitu bali kinakuongezea amani zaidi...so u shld 4get..
            Wednesday at 10:38am · LikeUnlike

            Adam Tibaigana Sinta kumbuka kila Binadamu ana mapungufu yake na pia Binadamu tumeumbwa kusahau mfano Sinta ukienda kilioni ukakuta mtu aliefiwa na mama yake anavyolia na khali aliyonayo kwa mawazo ya halaka huwezi amini kuwa mtu huyo ipo siku atakuja kusahau nakucheka. Hivyo sahau yaliyopita kwani kumbuka wakati yanatokea yale fikiria na umri muliokuwa nao ujana ndo ulichukua nafasi yake. SINTA FANYA KAZI NAE SAHAU YALIYOPITA.
            Wednesday at 10:44am · LikeUnlike

            Emmanuel Kimori Msamehe sintah,maandiko yanarema samehe mara 70,wewe msamehe bure. Mungu ndie wa kukulipa wewe kwa msamaha utakaoutoa c binaadamu.
            Wednesday at 11:00am · LikeUnlike

            Johari Luwembas Madua ndio kwa nini usiweze kusamehe ni dalili ya uungwana dadito
            Wednesday at 11:15am · LikeUnlike

            Ruben Mwakilima A
            Kama ni siku njema basi imefika maana HIYO NDIO KAULI NZURI ZAIDI KUISKIA IKIMAANISHA MUDA WA MABADILIKO, TIME TO CHANGE BECAUSE HAKUNA ADUI WA MILELE NA HAKUNA BINGWA WA MILELE NA HAKUNA ASIYE SAMEHE MILELE NA HAKUNA ASIYEKOSEA MILELE.... ...u nani usitake samehe? Mangapi UMEKOSEA MPAKA LEO KWA WENZIO NA BINADAMU YOYOTE? Wakati huu dada PESA NA UTU PAMOJA NA UBINADAMU MBELE... fanya Kazi NAYE (NATURE) na HEBU KAA NAYE OBE TABLE ONE SEAT NA MSHIKE MKONO ILI KAZI IWE POUA INGAWAJE USIFANYE AKAZANI UMEJIPENDEKEZA ILA MAELEWANO NA MAKUBALIANO MAANA NASI WABONGO HATUNA DOGO.... DHAMBI PIA KAMA UNAMCHUKIA MTU KWA MUDA MREFU SANA.... rudisha kiwango kwa UBAO MPYAAA MAANA PIA ITAUZA SANA HIYO... ujue ukweli ukimpenda sana DADAA AKAKUACHA "INAUMA SANA" alf Kama MZURI NDIO LAAAAAAAAAH ,WE JIANGALIE UTAGUNDUA ROHO INAUMAJE,LOVE HEALS ALSO... not only FOR PARTNERS BUT LOVE FOR ALL HEALSSee More
            Wednesday at 11:23am · LikeUnlike

            Mgaza Kossey kiukweli muda ule uliopita ulikuwa unaboa kila siku sinta sinta...may be unaweza kuanza upya na watu wakakupa shavu kiaina tofauti na zamani...jaribu kuanza upya hujachelewa!!
            Wednesday at 11:37am · LikeUnlike

            Fadhil Ally Uliyoyataka yameshaandikwa kwenye gazeti tayari, @sintah
            Wednesday at 11:41am · LikeUnlike

            Fadhil Ally Uliyoyataka yameshaandikwa kwenye gazeti tayari, @sintah
            Wednesday at 11:41am · LikeUnlike

            Fadhil Ally Uliyoyataka yameshaandikwa kwenye gazeti tayari, @sintah

            Isha Salum yaah....inawezekana mamtooo..ilikua zaman na sio ss.yaliyopita c ndwele angalien ya mbele..but kikaz tu. na c vingnevyo..sawasawa
            Wednesday at 11:45am · LikeUnlike

            Fadhil Ally Uliyoyataka yameshaandikwa kwenye gazeti tayari, @sintah
            Wednesday at 12:13pm · LikeUnlike

            Pamela Betabula mpz samehe yaliyopita kwanza hope umeshasahau yote maana ni muda sasa unajua ukisameheana na mtu unakuwa na amani sana fanya hiyo movie mpz itauza kishenzi
            Wednesday at 12:55pm · LikeUnlike · 1 personLoading...

            Leah Mafwenga uwiiii umenkumbusha mbali sana Christine Sintah jamani Rozana mhh angalia moyo wako unakuambia nini coz kusamehe kupo wangu
            Wednesday at 1:15pm · LikeUnlike

            Moses Killagane Dah yani nimekumbuka mbali sana enzi za SITAKI DEMU na INANIUMA SANA oooh my god.....heshimu maamuzi ya moyo wako si kuamua watakavyo watu wakati bado unaunia@sintah.
            Wednesday at 1:29pm · LikeUnlike

            Nancy Frank Samehe mara saba sabini kwani yule kaua itakua vizuri na utakua umefanya jambo la mbolea
            Wednesday at 2:00pm · LikeUnlike

            Sharifa Shafii ‎4gv and 4gt
            Wednesday at 2:12pm · LikeUnlike

            Albert Mganga Fanya kazi we mtoto achana na hizo maki2 coz deal kusaka mahela
            Wednesday at 2:32pm · LikeUnlike

            Albert Mganga Fanya kazi we mtoto achana na hizo maki2 coz deal kusaka mahela
            Wednesday at 2:45pm · LikeUnlike

            Kanju Ally mbona itakuwa full lmaisha nikusameheana tu na maisha mengine yanaendelea,hiyo k2 itabamba niaje me mwenywe lazima niitafute ni watch hiyo movie.
            Wednesday at 3:34pm · LikeUnlike

            Aniceth Tryphone Ngaiza Ynwa Yap unaweza nyote mmeshakua sasa mnajua nn kilitokea
            Wednesday at 4:29pm · LikeUnlike

            Sweetlips Bigkiss Sinta nakuomba ucheze hiyo movie kwani mimi ndiyo mmoja wapo wa watu tulioshirikiana na LAMATA kutoa mawazo hayo ya wewe kucheza movie na J. NATURE. N a mm ndiyo Location Manager wenu.
            Wednesday at 5:29pm · LikeUnlike

            Mwajuma Ndege Du hii kari nimekumbuka mbali sana tina but sshv umekua mamy yaliopita sindwele tugange yajayo itakua bomba wangu fanya kweli mdogo wangu mungu atakusimamia
            Wednesday at 5:40pm · LikeUnlike

            Lema Peter samehe tu yaliyopita si ndwele ganga yanayokuja
            Wednesday at 6:47pm · LikeUnlike

            Idd Minani
            Just let it go sinter have life countinue and move one with ur life never let past hold ur future people came to u and live u because his not joine in to ur body u must let him go and free ur mynd sinter his not part of ur body paty and it... ease to forgert abou him forgive and dont forget what hapen because that is memory ever single human have memory to remember if is good or bad that is how is it and that is fact u wont change See More
            Wednesday at 9:39pm · LikeUnlike

            George Kidubo what for bana hzo story za kzaman fanya ishu zngine za ukwel
            Wednesday at 9:48pm · LikeUnlike

            Kambi Mbwana Hakuna tatizo juu ya hilo, hivyo mnaweza kufanya kazi bila wasiwasi wowote.Naamini itakuwa ni film nzuri kupita kiasi, czwote mna vipaji na idadi kubwa ya mashabiki Tanzania. Sameheaneni, maana ndio ubinadamu huo.
            Wednesday at 11:08pm · LikeUnlike

            Leticia Thomas Pole mamii yaliyopita yamepita sahau fanya kazi
            Yesterday at 2:38am · LikeUnlike

            Leticia Thomas Pole mamii yaliyopita yamepita sahau fanya kazi
            Yesterday at 2:39am · LikeUnlike

            Irene Mkwizu Inawezekana kabisa my dear. Msamehe bure.
            Yesterday at 10:26am · LikeUnlike
          .
            Geko Jackson Kama kweli mkifanya kazi pamoja,hiyo movie ita hit sana bongo kwa sababu uhalisia utakuwepo
            4 minutes ago · Like