Pages

Pages

Monday, August 31, 2015

Sheria ya makosa ya mtandao kuanza kutumika rasmi kesho nchini Tanzania

 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam leo.Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini jijini Dar es Salaam leo.

Na Magreth Kinabo, Dar es Salaam

 SHERIA mpya   ya Makosa ya Mtandao ya mwaka   2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 zitaanza kutumika rasmi kesho Septemba Mosi mwaka huu, hivyo watumiaji   na watoa huduma waaswa kuzingatia sheria hizi ili kuepuka mkondo wa sheria.

 Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

“Sheria hizi ni nzuri zitaanza kutumika Septemba Mosi mwaka huu,kuanzia saa 6.00 usiku . zina maslahi katika nchi yetu. Ninatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi salama ya mtandao kwa manufaa yako na maendeleo ya Taifa letu,” alisema Profesa Mbarawa.

Bonanza la 10 la TASWA Arusha lafana, Taswa Queen waibuka mabingwa wa netiboli

Mchezaji wa Taswa Fc, Julius Kihampa (kushoto) akikokota mpira wakati wa mchezo wa Bonanza la 10 la Taswa Arusha dhidi ya timu ya IMS Maji ya Chai, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha mwishoni mwa wiki. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

Na Sufiani Mafoto, Arusha
TIMU ya Taswa Fc na ile ya Taswa Queens, zinazoundwa na wachezaji wa Habari za Michezo kutoka vyombo mbalimbali vya habari Tanzania, jana ilihitimisha ziara yake ya siku mbili katika mikoa ya Arusha na Tanga.
Aidha timu hiyo ilifanikiwa kumaliza ziara hiyo bila kufungwa huku Taswa Queens, wakiibuka kidedea kwa kutwaa Ubingwa wa mashindano ya Bonanza la Taswa Arusha yanayofanyika kila mwaka, baada ya kuwagalagaza bila huruma timu ya Chuo cha Waandishi wa Habari cha Arusha AJTC kwa jumla ya mabao 37-3. 
Mchezaji wa Taswa Queens, Oliver Arbogasti, akimdhibiti mchezaji wa timu ya Chuo cha waandishi wa Habari cha AJTC wakati wa mchezo wao. Katika mchezo huo Taswa Queens, ilishinda mabao 37 - 3

Unajua Dr John Pombe Magufuli amezaliwa lini? Soma hapa

VOTE on 25th October for CCM (Chama Cha Mapinduzi) Union Presidential candidate DR JOHN POMBE MAGUFULI.

Dr. John Pombe Magufuli

Dk. John Pombe Magufuli (amezaliwa 29 Oktoba 1959) ni mwanasiasa Mtanzania wa CCM ambaye aliwahi kutumikia Baraza la Mawaziri la Tanzania, kama Waziri wa Ujenzi tangu 2010. Hapo awali alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi tangu 1995 hadi 2000, Waziri wa Ujenzi tangu 2000 hadi 2006, Waziri wa Ardhi na Makazi tangu 2006 hadi 2008, na Waziri wa Mifugo na Uvuvi kutoka 2008 hadi 2010. Aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Chato tangu mwaka 1995. Yeye ndiye mgombea Urais wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Oktoba 25, chagua Dr John Pombe Magufuli na Samia Suluhu Hassan

Mchuano wa ubunge Moshi washika kasi


Red Brigade akiimarisha ulinzi katika viwanja vya Dkt Slaa mjini Moshi wakati wa uzinduzi wa Kampeni za mgombea Ubunge wa jimbo la Moshi mjini, Jafary Michael kupitia Chadema na Ukawa uliofanyika jana.
Baadhi ya viongozi na wagombea wa nafasi za Udiwani Kupitia Chadema na Ukawa.

Sunday, August 30, 2015

Helkopta ya Nyalandu yachengua mkoani Singida kwenye kampeni za CCM

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la  Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Na Joachim Mushi, Singida
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu amenogesha kampeni za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bi. Samia Suluhu katika mikutano yake inayoendelea ya kuinadi ilani ya CCM. Nyarandu ambaye jana alishuka kwa helkopta ya kukodi Jimboni kwake ikiwa ni muda mfupi baada ya mkutano wa kampeni kuanza alivuta hisia za wanaCCM na wananchi katika mkutano huo. Kama hiyo haitoshi mgombea huyo wa ubunge alitumia helkopta hiyo kwenye mikutano ya kampeni za mgombea mwenza ya Jimbo la Iramba Magharibi. Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kengege, Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida,
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuweka hadharani majina ya wapiga kura Visiwani Zanzibar Septemba 3 hadi 7

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba kuanzia tarehe 03/09/2015 hadi tarehe 07/09/2015 ili Umma uweze kupata nafasi ya kulikagua Daftari la Awali na kutoa taarifa za kufanyiwa marekebisho pale inapostahili.

Dr John Magufuli azidi kuchanja mbuga akiomba kura kwa Watanzania

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba. Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami, amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.

Amesema tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara  zaidi kilomita 7000 nchi nzima, ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka bilioni 73.3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.

Dkt MAGUFULI ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti  kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.

Aidha pia Magufuli  amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa  kumpa kura nyingi  zitakazomwezesha kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini.

Lowassa azoa mashabiki lukuki Jangwani jana kuzindua kampeni za UKAWA

Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani jana. Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.
Mke wa Mgombea Urais kupitia Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Mama Regina Lowassa akitoa salamu kwa wakazi wa Jiji la Dar Waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani jana.
Mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Duni Haji akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa Kampeni za Ukawa jana katika viwanja vya Jangwani.

Saturday, August 29, 2015

Chama Cha Mapinduzi CCM kinawashukuru Watanzania kwa kukiunga mkono chama chao

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinawashukuru sana Watanzania kwa kukiunga mkono chama chao hususan kwa wiki ya kwanza ya kampeni inayoendelea kutimua vumbi sehemu mbalimbali za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dr John Magufuli aenda kumjulia hali meya wa zamani wa jiji la Mbeya aliyepata ajali

 
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akimjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni,Mh Kapunga amelazwa kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa mjini humo.
 Mmoja wa Wauguzi walioko kwenye chumba maalum cha wagonjwa  mahututi (ICU), akimpa maelezo mafupi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu John Pombe Magufuli alipokwenda kumjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh. Athanas Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za maandalizi ya Kampeni hivi karibuni.

MGODI UNAOTEMBEA: Lowassa haaminiki, haeleweki, hafai kuwa rais wetu

NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM
UNAPOTAKA kuzungumzia jambo zito kama Uchaguzi Mkuu wa nchi, katu hupaswi kutanguliza ushabiki. Ushabiki ni mbaya mno. Unachochea kuaminisha watu ukweli wakati ni uongo. Kutafutwa rais wa nchi si kama mchezo wa kumbolela. Mchezo wa kombolela unaweza kuvunjwa wakati wowote na kuanza upya. Lakini si kupatikana rais, au kiongozi wa kuongoza taasisi nyeti kama Ikulu ya Tanzania.
Mgombea urais wa Chadema Mheshimiwa Edward Lowassa, pichani. Makamu wake ni Juma Duni Haji.
Tukifanya makosa katika kuchagua mtu mwenye weledi na nguvu ya kuitumikia nchi yetu na watu wake, hakika tutajilaumu kwa miaka mitano hadi 10 ijayo. Tutalia na kusaga meno. Ni kutokana na hilo, napinga kwa nguvu zote wote wanaochukulia kwa ushabiki Uchaguzi Mkuu wa Tanzania, wakiamini kuwa yule wanayemshabikia wao anapaswa kuwa rais. Si sahihi hata kidogo. Kwanini nasema hivi? Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na vikundi vya watu vinavyofanya kila wawezalo kuwaaminisha kwamba Edward Lowassa, anapaswa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Pombe Magufuli akiwa pichani katika moja ya mikutano ya kampeni inayoendelea nchini Tanzania. Makamu wa Rais wa Magufuli ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Vikundi hivyo vilianzia harakati zao tangu akiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Vikundi hivyo vilisumbua mno. Vilichanganya wengi na kuwaaminisha kutokana na ushabiki wao na nguvu ya kimkakati, sanjari na uwezo wao wa kifedha, hivyo kutaka aungwe mkono kwa udi na uvumba. Pamoja na ushabiki huo, lakini mgombea wao Lowassa hajaweza kuvuka viunzi vya NEC ya CCM, mjini Dodoma. Bila kuangaliwa usoni, Lowassa alikatwa. Siku moja baada ya kukatwa, vikundi hivyo hivyo vikaanza kubadilisha wimbo wa nguvu ya mtandao wa CCM na kuihamishia kwenye upinzani, ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Nguvu hiyo ikawashinda akina Freeman Mbowe na wenzake waliokuwa wakipita huku na kule kuaminisha watu kuwa Lowassa ni fisadi, hapaswi kuachwa atembee barabarani kwa matao hali ya kuwa ameifisadi nchi yetu.

Hatimae wimbo wa ufisadi wa Lowassa ukazimwa, ukaanza kuimbwa mwingine wa mfumo mbovu wa CCM. Ati mfumo ndio tatizo. Tatizo si la Lowassa tena. Wimbo huu wa mfumo ndio unaoimbwa sasa. Kila mtu anaimba huo, ukianzia kwenye vinywa vya wana mtandao wake. Hata hivyo, bado haiwezi kukwepeka kusema kwamba kama tatizo ni mfumo, Lowassa hawezi kukwepa lawama hizo. Hii ni kwa sababu aliitumikia nchi kwa miaka zaidi ya 35. Alikuwa ndani ya chama cha CCM na Waziri Mkuu pia. Hizo ni nafasi nyeti na kubwa mno zilizokuwa kwenye mfumo huo huo.

Friday, August 28, 2015

Muone Mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan alivyomvaa mgombea udiwani wa Chadema mkoani Arusha

"MWAKA HUU MTAISOMA NAMBA" Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani akimwambia Mgombea Udiwani wa Chadema, Anna Oloiwa, aliyefika kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza huyo, uliofanyika eneo la Madukani, Longido mkoani Arusha leo.

Kutana na kijana mwenye ndoto ya kuwa kama Mohamed Dewji

04.jpgk
Mfanyabiashara wa Kimataifa Abbas Maziku akiwa katika picha ya pamoja na Mfanyabiashara ambaye pia ni Bilionea kijana Barani Afrika, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji, 'MO' amabaye anafuata nyayo zake katika kufikia malengo yake kibiashara.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BIASHARA ya kusafirisha mazao ni miongoni mwa biashara zenye ushindani mkubwa kutokana na kutawaliwa na matajiri wenye asili ya Kiasia.
Kutokana na sababu hiyo imewafanya waafrika wengi kuwa na uthubutu katika biashara kwa kuhofia huenda wasifanikiwe na kujitanua kibiashara.
Mbali na ugumu huo lakini pia waafrika wengi hasa watanzania wamejikuta wakiishia kuwa wafanyabiashara ya kawaida na kupoteza fursa za kimataifa .
Kupoteza fursa muhimu za kimataifa kumefanya wakose fursa ambazo zingeweza kuwafanya wawe na mawazo mengine ya kuchangamkia fursa za kibiashara na kufikiri nje ya boksi.
Makala haya ndani ya mtandao huu yanaangazia mahojiano na mfanyabiashara wa kwanza wa kitanzania kufanya biashara ya kusafirisha Korosho kwenda nchini Vietnam aitwaye Abbas Maziku ambapo alielezea alipoanzia, vikwazo, mafanikio na matarajio yake kibiashara.

Alipoanzia

Maziku anasema alianza biashara ya kusafirisha mazao mnamo mwaka 2013 baada ya kuvutiwa na mjomba yake ambaye alikuwa na mashamba yaliyokuwa na mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao ambayo Maziku alianza nayo na anaendelea nayo ni pamoja na Korosho, Ufuta, Mbaazi, Choroko, Mtama, Alizeti, Mashudu yapamba na pamoja na Pilipili Manga.

Mgombea urais wa Chadema Edward Lowassa alipokutana na wanawane jijijini Dar es Salaam jana

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono baadhi ya Wanawake wanachama wa CHADEMA, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam jana Agosti 27, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwasalimia baadhi ya Wanawake wanaounda Baraza la Wanawake wa Chadema, waliokuwa wamefurika kwa wingi nje ya Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam, wakati walipowasili kwa kuhutubia Baraza hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWICHA), Mh. Halima Mdee akizungumza na Umati wa Kinamama wa Chama hicho, uliokuwa umefurika kwa wingi nje ya Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la LAPF, Millennium Tower,  Kijitonyama jijini Dar es salaam jana Agosti 27, 2015, kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Baraza hilo, uliohutubiwa na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

Ukiwa na haraka Mbweni JKT jiandae kupiga mbizi

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UPIGE mbizi. Ndivyo unavyoweza kusema msemo huu kama unahitaji kupita haraka haraka katika eneo la Mbweni JKT, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mahala panapojengwa daraja la kuvukia watu kwa miaka mitatu sasa, halina dalili za kukamilika hivi karibuni. Ni eneo tata. Ni eneo linalokera na kusumbua watu mno. Mbaya zaidi, ni eneo lililozunguukwa na majumba ya watu wenye ukwasi au ukubwa wa majina ya viongozi waliojenga katika eneo hilo. Eneo linalojengwa daraja hilo ni kwenye mkondo wa maji unaotokea baharini.
Gari likivuka eneo la mkondo wa bahari, ambapo pia ndipo panapojengwa daraja hilo hatua chache mkono wa kulia kutoka gari linapopita. Maji yakijaa hapo hakuna kupita wala kuvuka.

Kwa wanaofahamu tabia za mikondo hii ya baharini watakuwa wanaelewa. Na wasiofahamu ni kwamba, linakuwa na tabia za kujaa maji na kupungua kila wakati. Kwa mfano, mtu anaweza kupita saa tatu asubuhi akakuka hakuna maji mengi. Lakini dakika kadhaa mbele, maji mengi yanajaa kutokea baharini. Ukifanya mkosi, ukiwa na haraka ya kuendelea na shughuli zako, ndipo hapo unapopaswa upige mbizi.
Hapa ndipo panapojengwa daraja hili.
Uyavulie nguo, upite. Na ikiwa na una gari, huna budi kusubiri kwanza yapunguwe kama si kuisha kabisa maji hayo. Au utafute njia nyingine za kukufikisha eneo unaloelekea, ingawa njia hiyo ina usumbufu mkubwa wa muda na gharama nyingine pia. Ni kutokana na hilo, serikali kwa kupitia Halmashauri ya Wilaya Kinondoni, inapaswa kupigia jicho kuu eneo hili. Iangalie tatizo ni nini? Mbona daraja hilo halikamiliki kwa miaka mingi sasa. Hakuna kinachoendelea. Watu wanapata tabu. Mbaya zaidi ni eneo linalovutia na kusisimua, maana haiwezekani mtu ajenge nyumba mamilioni ya shilingi wakati njia ya kumfikisha kwake haieleweki eleweki. Ni wazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni pamoja na DC Paul Makonda wanapaswa kuliangalia suala hili kwa kina.

Thursday, August 27, 2015

Mgambo waendelea kukaangwa, CCM yasema mwisho wa kusumbua wafanyabiahara wadogo umefika

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru. Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, akihutubia Jimbo la Arumeru, 

Joachim Mushi, Arusha
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha mgambo wa halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa kamatakamata za wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama pamoja na vijana.

Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano uliofanyika uwanja wa Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na wananchi wengine.

Akinadi ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za akinamama na vijana wanaojitafutia ridhiki mjini.

Bondia wa kike wa Tanzania Lulu Kayage akwea pipa tena kumfuata Lizberth Afrika Kusini


BONDIA wa Kike Lulu Kayage pichani, ameenda tena nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya mpambano wake mwingine na bondia mwingine kutoka uko utakaofanyika Agosti 28 nchini Afrika ya Kusini.

Akizungumza kabla ya kupanda ndege bondia huyo alijigamba kuwa ataenda huko na atashinda kwa kuwa yupo fiti zaidi kwa sasa, hivyo ataendeleza wimbi la ushindi sambamba na duwa kwa Watanzania wamuombee ili aweze kumchakaza mpinzani wake Lizbeth Sivhag.

Na Mwandishi Wetu

Bondia huyo aliyeambatana na bondia mkongwe wa siku nyingi George Sabuni kwa ajili ya kumkumbusha mambo mbalimbali awapo ulingoni.

Magufuli aendelea kuchanja mbuga Tunduma, ajaza nyomi ya hatari

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema jana mchana, kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano, ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25  mwaka huu.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mlemavu wa miguu ndugu Joseph, mkazi wa kijiji cha Lwasho wilaya ya Momba,ambapo alimuahidi kumletea baiskeli ya kutembelea.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli  akiombewa na Watawa wa kijiji cha Lwasho,mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni katika kijiji cha Lwasho,wilaya ya Momba.

Wednesday, August 26, 2015

Madaktari Bingwa wa Moyo toka India , wanatarajiwa kupambana na ugonjwa wa moyo kwa watoto



Na Mwandishi Wetu ,
Kutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki. Takriban watoto 8 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani Afrika inaweza kuwa wengi sana.

Watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa. baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu, mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo, kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara. Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha ‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko upumuaji.

Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Paul Makonda, azindua tawi jipya la benki ya First National Bank Mbezi Beach jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam huku akiambatana na Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo na Mkuu wa Huduma za Rejareja wa benki hiyo, Francois Botha.
Mkuu wa Bidhaa na Huduma za Mitandao, Silvest Arumasi akimpa maelekezo Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda mara baada ya kufungua rasmi tawi la benki ya First National la Mbezi Beach jana jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Balozi wa Heshima wa Djibouti Said Shamo.

Dr Magufuli atambulishwa Sumbawanga na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye mbio za kusaka urais

 Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, Mhe. Mizengo Pinda akimtambulisha mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya uwanja wa Nelson Mandela jana jioni.
   Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sumbawaga mjini mkoani Rukwa,ndani ya Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mkutano wa kampeni,pichani nyuma ni Waziri Mkuu Pinda akishuhudia tukio hilo.

Tuesday, August 25, 2015

MGODI UNAOTEMBEA: Filamu ya Edward Lowassa haina uhalisia kwa Watanzania masikini

NA KAMBI MBWANA, DAR ES SALAAM
INASHANGAZA na kustaajabisha mno. Maisha ya Watanzania yanapotaka kuingizwa mtegoni kutokana na tamaa za watu wachache walioungana kwa ajili ya kuitafuna nchi. Hii ni hatari zaidi ya hatari ya kukutana na simba mwenye njaa kali. Ndivyo unavyoweza kusema unapotaka kuelezea aina ya siasa za Mgombea urais wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Edward Lowassa. Lowassa anayeonyesha kuwa ana njaa kubwa ya kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
 Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa kushoto akiigiza kutoa nauli ya daladala alipokuwa kwenye ziara yake jana jijini Dar es Salaam.
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli akizungumza katika ufunguzi wa kampeni zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam.

Si dhambi kuwa na kiu ya kuwa mtawala, ila mbinu zinazotumika ndio zinazotia mashaka. Wajuzi wanajiuliza bila kupata majibu sahihi. Tangu alipokuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lowassa amekuwa akitumia nguvu kubwa. Haswa nguvu ya kifedha. Amekuwa akinunua makundi ya watu ili wamuunge mkono. Ingawa wapo wanaomuunga mkono kwa mapenzi yao, lakini robo tatu ya hao wenye mapenzi nao, hakika wanavutwa na mbinu nyingine, zikiwamo hizo za fedha.

Hilo ndio tatizo lake. Na ili kuonyesha kwamba anakubalika, vikundi hivyo vinavyomuunga mkono, ndivyo vinavyokaa na kutunga hadithi, filamu za kuaminisha kukubalika kwake. Mapema wiki hii, siku ya Jumatatu, Lowassa aliibukia kwenye daladala za Gongolamboto.
Eti amekwenda kujifunza jinsi maisha ya Watanzania wengi wa jijini Dar es Salaam wanavyoishi katika suala zima la usafiri. Ndio, watu wanaishi kwa tabu. Na pengine suala la usafiri jijini Dar es Salaam ni tatizo kubwa. Wengi wanapoteza muda barabarani. Foleni zisizoeleweka au hata kuingilia dirishani kwa wingi wa wawahitaji wa daladala hizo.

Hata hivyo Lowassa ameshindwa kupata uhalisia wa adha hizo. Hii ni kwa sababu kwanza amekaa kwenye kiti cha daladala na kusubiri apigwe picha. Hii inaonyesha ni tukio la kupangwa na pengine hata hao wenye daladala walijua kinachoendelea na walimuwekea mazingira mazuri bwana mkubwa wao huyo anayependa ujiko, sifa. Kama huu ni uongo, basi upo karibu na ukweli. Najiuliza tu, huyu mtunzi wa filamu ya Lowassa juu ya daladala aliyokwea, hakujua kwamba adha kubwa ipo alfajiri na zaidi daladala za Mbagala, Kimara, Mbezi? Nashawishika kusema kwamba dereva wa daladala lenye usajili T 917 CWS pengine na konda wake walijua kila kinachoendelea na wao walilipwa ujira wao.

Onesmo Ngowi ampa tafu ya vifaa vya masumbwi bondia Lulu Kayage

Rais wa I.B.F Africa Onesmo Ngowi kulia akimkabidhi vifaa vya mchezo wa ndondi bondia Lulu Kayage baada ya kutembelea ofisi za rais huyo zilizopo posta Dar es salaam Lulu Kayage ataondoka nchini kuelekea Afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wake mwingine kabla ya kugombania ubingwa wa I.B.F Afrika mnamo Desemba 2 mwaka huu.

Rais wa I.B.F Africa Onesmo Ngowi wa pili kulia akiwa na bondia Lulu Kayage wa pili kushoto kulia ni George Sabuni na kushoto ni Hamisi Berege.

Benki ya Mkombozi yafungua tawi jipya Moshi

Baadhi ya wananchi wakishuhudia ufunguzi rasmi wa Benki ya Mkombozi tawi la Moshi.
Askofu wa jimbo Katoliki la Moshi ,Mhashamu Baba Askofu Isaac Amani akimwaga maji ya baraka katika jingo la Benki ya Mkombozi tawi la Moshi.

Dk Magufuli ni hatari, afanya balaa Katavi akiomba kura za kugombea urais

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli akihutubia wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi.

Copy the BEST Traders and Make Money (One Click) : http://ow.ly/KNICZ

 Waziri Mkuu MizengO Pinda akimtambulisha Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli mbele ya umati wa watu waliofurika jioni ya leo kwenye uwanja wa Azimio mjini MPanda mkoani Katavi wakati wa muendelezo wa kampeni za chama hicho mkoani humo leo.Chama cha CCM kimezindua kampeni zake jana katika viwanja vya Jangwani jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama na wakereketwa wa chama hicho cha CCM
 Wananchi wakishangilia wakati  Waziri Mkuu Pinda alipokuwa akimnadi Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, John Magufuli  wakati wa mkutano wa kampeni katika Uwanja wa  Azimio mjini Mpanda, mkoani Katavi.

Monday, August 24, 2015

TANAPA yaanzisha kampeni kabambe ya miezi sita ya kuhamasisha utalii


Kaimu Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketansi akizungumza na wanahabari(hawako pichani) juu ya Kampeni ya uhamasishaji wa utalii wa ndani kwa wazawa itakayodumu kwa muda wa miezi sita.


Baadhi ya Maofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wakizungumza na wanahabari (hawako pichani ) juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa ambapo katika kipindi cha miezi sita watakao tembelea zaidi ya Hifadhi nne watapata ofa ya kutembelea Serengeti ikiwa ni pamoja na kugharamiwa maradhi katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano.