Wadau wa Elimu, Abdulaziz Jaar kulia, akizungumza jambo katika matembezi ya Shule ya Kiislamu ya Twayyibat Islamic Seminary ya Temeke jijini Dar es Salaam. Katikati ni mdau kutoka Yukubu Chamber&Associate.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKUU wa wilaya Temeke, DC Sophia Mjema, ameipongeza shule ya
Sekondari ya Kiislamu inayojulikana kama Twayyaibat Islamic Seminary Secondary
School kwa kufanya ada nafuu inayoweza kuwafanya wazazi na walezi wamudu
gharama za kusomesha watoto kwenye shule binafsi.
mwanafunzi kutoka Twayyibat Islamic Seminari akisoma Quraan katika shule hiyo walipotembelewa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, hayupo pichani.
DC Mjema aliyasema hayo alipofanya ziara katika shule hiyo na
kukuta uongozi wa Twayyaibat, ukitoa ada ya Sh 200,000 tu kwa mwaka, jambo
ambalo ni agharabu mno hususan kwa shule za kulipia na zinazomilikiwa na
taasisi za kidini.
Akizungumza kwa mshangao mkubwa mbele ya wadau wa elimu, DC
Mjema alisema ameshangazwa na shule hiyo kufanya ada nafuu, hivyo ni jukumu la
wazazi na walezi kujitokeza kuwasomesha watoto wao kwa nguvu zote.
Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia akimkabidhi cheti Mr Yakubu kwa kutambua mchango wake kwa maendeleo ya shule ya Twayyibat Islamic Seminary, iliyopo Temeke, jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Skywadrs Construction, Saeed Pirbaksh Mulla, akipokea cheti cha kutambua mchango wa kampuni yao kwenye shule hiyo. Cheti hicho anakabidhiwa na Mkuu wa Wilaya Temeke, Sofia Mjema, kulia.
Alisema pamoja na ada hiyo kuwa nafuu, ni jukumu la serikali
hususan Halmashauri ya Wilaya Temeke kupanga mbinu bora zinazoweza kuisaidia
shule hiyo kwa hali na mali ili waweze kufanya kazi ya kutoa elimu kwa kiwango
cha juu.
“Hii naweza kuiita shule ya sekondari ya mshangao hasa baada
ya kuona unafuu wa ada yake, nikiamini kuwa Dunia ya leo kukuta unafuu wa namna
hii unaonyesha namna gani kuna wadau wana mtazamo wenye maendeleo.