https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, December 29, 2016

Rais Magufuli ashiriki msiba wa mzee maarufu Chato

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole   Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita. Picha kwa hisani ya IKULU

Monday, December 26, 2016

Kompyuta za Bayport zaifuta machozi Halmashauri ya Same

Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kulia), akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick moja ya kompyuta sita zilizotolewa na taasisi yao kwa mkoa huo kama msaada wa kuweza kuongeza utendaji kazi mzuri kwa watumishi wa umma, hususan kwa Manispaa ya Moshi, Halmashauri ya Mwanga na Halmashauri ya Same, huku kila moja ikipewa kompyuta mbili. Kushoto kwa RC Sadick ni Katibu Tawala wa Mkoa huo wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Aisha Amour. Picha zote na Mpiga Picha Wetu. 

Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
HALMASHAURI ya Wilaya Same imeanza kupokea faraja za msaada wa kompyuta mbili kati ya sita zilizofikishwa mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi yao kuungua moto na kutekeza vifaa mbalimbali vya kiofisi.

Kompyuta hizo zilipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick, akiambatana na wakuu wa idara wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na watumishi mbalimbali kutoka kwenye halmashauri za Same na Mwanga.
Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Mheshimiwa Said Mecky Sadick wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta hizo alizopokea kwa Taasisi ya Bayport Financial Services, Katibu Tawala wake wa Mkoa, Mheshimiwa Aisha Amour.


Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya kupokea kompyuta hizo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamekabidhi kompyuta hizo, ikiwa ni siku chache baada ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Same kuungua moto.

Alisema ingawa msaada wao umekuja kabla ya ofisi hizo kuungua moto, lakini wanaamini kuwa kompyuta hizo zinaweza kupunguza adha ya watumishi wa umma kufanya kazi kwa wakati mgumu, huku zikilengwa kwa Halmashauri ya Same, Mwanga na Manispaa ya Moshi.

Marehebu Mpoki Bukuku alivyoagwa jijini Dar es Salaam

 Wanahabari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku baada ya kutolewa heshima za mwisho katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam, tayari kulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiwaongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mpigapicha Mwandamizi wa The Guardian, marehemu Mpoki Bukuku katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Tabata, Dar es Salaam. Mwili wa Mpoki ulisafirishwa kwenda kwao Msalato Dodoma kwa mazishi.
 Mwenyekiti wa Chadema, Freeman  akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mpendwa wetu Mpoki Bukuku.

Watumishi mbalimbali wa madhehebu washauriwa kusaidia yatima

 Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiombea  bajeti mbalimbali  za waumini walizoziletwa kwa ajili ya kutolewa neno la unabii hiii leo(picha na woinde Shizza wa libeneke la kaskazini Arusha).

Habari picha na woinde shizza,Arusha
 Watumishi  wa madhehebu mbalimbali hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kuwasaidia yatima ili nao waweze kujisikia kama wao ni sehemu ya jamii

Hayo yamebainishwa leo na Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie wakati akifanya  dua maalumu ya kupitisha bajeti ya watu walioshiriki katika sikukuu ya kukusanya iliyofanyika katika hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha.
Nabii mkuu mheshimiwa Dr Geordavie akiwa anahubiri katika
hema la kukutania ngurumo ya upako kisongo jijini Arusha hii leo.

Sunday, December 25, 2016

Maonyesho ya kahawa na utalii yafanyika kwa mafanikio nchini Saudi Arabia

 Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, mwenye suti nyeusi akifanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa biashara katika maonyesho yaliyofanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia.


Na Mwandishi Wetu, Riyadh Saudi Arabia
Maonesho makubwa ya kahawa na chocolate (coffee and Chocolate) yamemalizika kwa mafanikio jijini Riyadh Saudi Arabia, huku kwa mara ya kwanza maonyesho hayo yakishirikisha Ubalozi wa Tanzania, nchini Saudi Arabia. Katika maonyesho hayo yaliyoanza Desemba 20 hadi 23 mwaka huu, yalihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyabiashara wa Tanzania kwa nia ya kutangaza bidhaa za mazao ya kilimo na viwanda kutoka Tanzania.


Akizungumza katika maonyesho hayo, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, aliyasifu maonyesho hayo akisema kuwa yamekuwa na tija kwa nchi ya Tanzania pamoja na wafanyabiashara waliohudhuria. Alisema ofisi yake ilidhamilia kuyatumia maonyesho hayo kwa ajili ya kutangaza bidhaa za Tanzania pamoja na wafanyabiashara wake ili kufanikisha maendeleo yao kwa ujumla kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao.
 Mazungumzo yanaendelea kwenye banda hilo.
 Balozi Hemed Mgaza akizungumza na wawekezaji wa Saudi Arabia waliohudhuria katika maonyesho hayo.

Thursday, December 22, 2016

Arusha wafurahia kompyuta za Bayport

 Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya mikopo ya Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kushoto), akimkabidhi Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Emelda Kisosi,  kompyuta kwa ajili ya kusaidia ufanisi wa kazi ofisi zao kama sehemu ya kujitolea kwa jamii. Kulia ni Ofisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Edna Mwaipiana. 

Na Mwandishi Wetu, Arusha
HALMASHAURI ya Wilaya Arumeru, mkoani Arusha, jana imepokea kompyuta mbili zilizotolewa msaada na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kama sehemu ya ushirikiano na kusaidia na kukuza ufanisi wa kikazi kwa watumishi wa umma wilayani humo.

Kompyuta hizo zinatoka ikiwa ni siku chache baada ya Mkoa wa Morogoro nao kupokea msaada kama huo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa katikati akizungumza jambo katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Kulia ni Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Emelda Kisosi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo leo jijini Arusha, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamefikisha kompyuta mbili katika wilaya hiyo kama orodha ya mahitaji waliyopokea kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. 

Alisema anaamini kwa kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kutatibu na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kiutendaji wakati wote.

Tuesday, December 20, 2016

Jeshi la Polisi lamkamata mtuhumiwa wa utapeli jijini Dar es Salaam

Msemaji wa Polisi, Advera  Bulimba – ACP


Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

JESHI la Polisi nchini limefanikiwa  kumkamata mtuhumiwa wa utapeli anayejulikana kwa jina la  Wilfred Masawe (36) , Kabila mchaga na  mkazi wa  Buza, Temeke jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Dar es Salaam leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidi wa Polisi (ACP), Advera  Bulimba amesema  mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mbinu mbalimbali kutapeli zikiwemo kujitambulisha kama kiongozi wa serikali kwa kutumia mtandao wa Whatsapp,  huku akieleza kuwa yupo nje ya nchi na kuna tatizo la msiba ambao umetokea nchini na unamuhusu na hivyo alikua akitoa maelekezo kwa watendaji wa serikali waweze kusaidia gharama za matibabu hospitalini, gharama za kusafirisha mwili wa marehemu na gharama za mazishi.


Alisema pia alikuwa akitumia mbinu ya kujifanya kiongozi mkubwa wa dini ya kikristo (Askofu) na kuwaambia waumini na viongozi mbalimbali kuhusu maandalizi ya makongamano ya kidini kwa lengo la kuwaomba michango kuweza kufanikisha makongamano hayo.

Uelewa kuhusu Saratani waongezeka kwa akina mama

Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na masuala ya afya pamoja na ukatili wa kijinsia kwa vijana na wanawake nchini la Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Elizaberth Ndakidemi, akizungumza hii leo wakati wa mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza, unaotekelezwa na shirika hilo.
#BMGHabari
Wadau wa afya mkoani Mwanza, wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la TAYOA, Elizaberth Ndakidemi, wakati akizungumza kwenye mkutano wa kushirikishana uzoefu, changamoto pamoja na mafanikio katika utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa Saratani ya shingo ya kizazi mkoani Mwanza.

Waajiri waaswa kuwasilisha michango ya wafanyakazi Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi

Na Anthony John, Globu ya Jamii
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi ,vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewataka waajili wote kuwasilisha Michango ya wafanyakazi wao Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwa wakati.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Mhe. Jenista Mhagama, akihutubia kwa niaba ya Waziri Mkuu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Muhidin Sufiani.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Huduma za utoaji wa Mafao ya fidia kwa wafanyakazi na ubia kati ya Mfuko na watoa Huduma za Afya amesema kuwa 
kwa Mwaka huu wafedha Serikali imewasilisha Michango ya wafanyakazi wake wote ambapo alizitaka Sekta binafsi pia kuwasilisha Michango yao kwa wakati.

Sanjari  na Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mshomba ameongeza kuwa Mpaka kufikia Novemba 30 Mwaka huu Jumla ya waajili 5945 wamechangia na wamepewa na ya usajili.

Hata Hivyo Mweketi  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo Emmanuel Humba amesema Mfuko Huo utachangia kwa kiwango kikubwa Sera ya Tanzania ya Viwanda  iliyoa anzishwa na Serikali ya awamu ya tano kwani wafanyakazi watakapo  kuwa na Afya njema watafanya kazi kwakujiamini na kuleta Maendeleo.

Kompyuta za Bayport zafikishwa kwa ofisi za Mkoa wa Morogoro

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto, akimkabidhi moja ya kompyuta sita zilizotolewa na Taasisi yao kwa ajili ya kuusaidia Mkoa wa Morogoro katika vifaa vya ofisini ili kurahisisha utendaji kazi. Anayepokea ni Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe, leo mkoani Morogoro. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo imekabidhi kompyuta sita kwa uongozi wa Mkoa wa Morogoro, kwa kupitia Mkuu wake wa Mkoa, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe, ili zisaidie utendaji kazi wa watumishi wa umma katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya Mvomero, Manispaa ya Morogoro Mjini pamoja na Morogoro Vijijini.

Ugawaji wa kompyuta hizo ni mwendelezo wa taasisi hiyo kugawa vitendea kazi hivyo baada ya kumkabidhi kompyuta 125 kati ya 205 kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki, huku kompyuta zote zikiwa na thamani ya Sh Milioni 500.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo mwenye miwani akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe mwenye suti nyeusi. Kulia kwa Cheyo ni Afisa Tawala wa Mkoa Morogoro, Victor Ndiva na nyuma ni Mercy Mgongolwa, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services.
Hapa ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo mwenye miwani akipiga picha ya furaha na Mkuu wa Mkoa Morogoro, Mheshimiwa Dkt Stephen Kebwe mwenye suti nyeusi. huku akiwa ameshikana mkono na Afisa Tawala wa Mkoa Morogoro, Victor Ndiva. Nyuma kwa Cheyo ni Mercy Mgongolwa, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services.

Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba wamejisikia furaha kufikisha vitendea kazi hivyo kwa serikali ya mkoa wa Morogoro.

Alisema taasisi yao inafanya kazi ya utoaji wa mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa pamoja na ile mikopo ya viwanja kwa Watanzania wote, wakiwamo wajasiriamali.

Monday, December 19, 2016

Mashindano ya Mamlaka ya Bandari Tanga yafikia tamati


Kapteni wa timu ya Bandari Tanga, Abdalla Abdulla, akipokea Kombe la Ubingwa wa jumla na Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana mara baada ya kumalizika michezo hiyo iliyoshirikisha timu za Tanga, Dar Makao Makuu, Mtwara na Bandari za Maziwa.

Na Mwandishi Wetu, Tanga
Tanga, MICHEZO ya tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) yamemalizika kwa timu ya Bandari ya Tanga kuibuka Mabingwa wa jumla.
Timu ya Bandari ya Tanga imeibuka kwa kunyakua vikombe 7 ikifuatiwa na Bandari Makao Makuu Dar es Salaam kwa kujinyakualia vikombe 7 ambapo Bandari Mtwara na Bandari za Maziwa kila mmoja kujinyakulia kikombe kimoja kimoja.

Akikabidhi vikombe na zawadi mbalimbali kwa washindi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana ,aliwapongeza washiriki hao kwa kuonyesha umahiri katika michezo mbalimbali. Alisema mbali ya umri wao kwenda juu lakini walikuwa wakionekana kama vijana ambao wanaweza kucheza timu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.

“Nimefarijika kuwaoma wafanyakazi wenzangu umri tofauti mukicheza mpira na kushindwa kutofautisha kijana na mzee, munakimbia uwanjani kama Messi na Ronaldo” alisema Msabimana. Aliwataka wanamichezo hao ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kuwa wamoja na kuwa na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea.

Viwangp vya watoto wachezao mchezo wa golf vyazidi kupanda

Na Luteni Selemani SemunyuViwango vya Watoto wanaocheza mchezo wa golf katika klabu ya Jeshi la Ulinzi la  Wananchi wa Tanzania ya Lugalo vinazidi kupanda na kuongeza uwezekano wa  kupata vipaji vipya  na Wawakilishi wa Taifa.
Mshindi wa mashindano maalum ya watoto yaliyoandaliwa na klabu ya Golf ya JWTZ ya Lugalo, Habiba Likuli akipiga mpira huku wachezaji wenzake wakimuangalia katika hekaheka za mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Luteni Selemani Semunyu)

Hayo yalisemwa na Mmoja wa Walimu wa Mchezo huo wa Klabu ya Lugalo Elias Chiundu mara baada ya mashindano ya Watoto yaliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waaandishi wa habari mwalimu huyo alisema yeye kama Mwalimu anafarijika kwa kuona viwango vya watoto hao vikikua na hivyo ni matarajio yake katika mwaka 2017 watafanya vyema Zaidi.
Mshindi wa pili wa mashindano maalum ya watoto yaliyoandaliwa na klabu ya Golf ya JWTZ ya Lugalo, Sophia Juma, akipiga mpira huku wachezaji wenzake wakimuangalia kwenye mashindano hayo.

“Mwaka 2017 tunataraji baadhi ya watoto  waliokuwa wanacheza katika Daraja la Junior kutokana na Umri wao kuongezeka sambamba na kiwango cha uchezaji basi wataingia katika Divisheni Nyingine na kutoa changamoto kwa waliowakuta” Alisema Chiundu.
Aliongeza kuwa kuna Faida kubwa kwa Wachezaji kuandaliwa wangali wadogo kwani wanakuwa na kipindi kirefu cha  mafanikio iwapo wataweka jitihada sambamba na kuungwa mkono na wazazi.

Thursday, December 15, 2016

Kada wa CCM Emmanuel Shilatu ampongeza Dr Magufuli


CCM MPYA YA HAPA KAZI TU

Napenda kuungana na mamilioni ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kumpongeza Mwenyekiti wa chama Taifa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuja na CCM mpya yenye dira na maboresho zaidi ya kurudi kwenye misingi ya uasisi wa CCM. Ni CCM ya "Hapa Kazi Tu".

Kila mtu amefurahia kwa namna Mwenyekiti Dk. Magufuli alivyoibuka na mikakati ya Mwanachama kukifuata chama na sio mtu, kupunguza idadi ya vikao, kuja na utaratibu wa kadi za kielektroniki utakaondoa utitiri wa kadi feki, kupunguza kitendo cha mtu kumiliki cheo zaidi ya kimoja, kupunguza idadi ya wajumbe kamati kuu na wajumbe wa NEC.

Maboresho hayo yamekisogeza chama kwa wanachama jambo litakalotoa fursa kukua kwa chama kimuonekano, kivitendo, kimtazamo kutokana na chama kuwa mali ya wanachama wote.

Halikadhalika nampongeza Mwenyekiti wa CCM Dk. Magufuli kuja na uteuzi makini wa Ndugu Rodrick Mpogoro (Naibu Katibu Mkuu - Bara) Humphrey Polepole (Katibu Itikadi na uenezi), na Kanali Ngemela Lubinga ( Katibu wa NEC siasa na uhusiano wa kimataifa. Hawa wote walioteuliwa ni watu makini, weledi, sahihi kabisa waliokuja kwa wakati sahihi. Kiukweli wametosha katika nafasi zao.

Rai yangu kwa wanachama ni wakati sasa kuacha kutafuta vyeo kwa njia za kutoa rushwa, mwanachama kukifuata chama na si mtu, uwekezaji kufanywa kwa chama na si wanachama, wanachama kufanya kazi ya kukijenga chama na kuhakikisha chama kinarudi katika misingi yake iliyojengwa na waasisi wa chama chetu ambacho ni kimbilio kwa wafanyakazi na wakulima.

Kiukweli tarehe 13/12/2016 CCM ilizaliwa upya tena. Hongera sana Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli, wajumbe wa Kamati kuu, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuja na CCM mpya, CCM ya hapa kazi tu.

Tuesday, December 13, 2016

CCM kufanyika mabadiliko makubwa, DC Polepole arithi mikoba ya Nape Nnauye

TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. John Pombe Magufuli.
Mikoa ya Bara 26x1 = 26
Mikoa ya Zanzibar 6x1= 6
Mikoa ya Bara 26x1= 26
Mikoa ya Zanzibar 6x4= 24
Kutoka Bara = 15
Kutoka Zanzibar =15
UWT= 5
WAZAZI= 5
Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni =5
Mwenyekiti wa CCM= 1
- Makamu Mwenyekiti (B)= 1
-Makamu Mwenyekiti (Z)= 1
- Makamu wa Rais = 1
- Waziri Mkuu = 1
- Makamu wa Pili wa Rais (Z) =1
- Spika wa Bunge = 1
- Spika wa BLW = 1
- Mwenyekiti wa UWT= 1
- Mwenyekiti wa WAZAZI=1
-Mwenyekiti wa UVCCM =1
- Katibu Mkuu – WAZAZI =1
- Katibu Mkuu – UWT = 1
- Katibu Mkuu – UVCCM = 1
Jumla: 158
#.Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vitafanyika kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
Makamu wa Rais
Katibu Mkuu wa CCM
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa Pili wa Rais (Z)
Spika wa Bunge la Tanzania
Spika wa BWL
Mwenyekiti wa WAZAZI
Mwenyekiti wa UWT
Mwenyekiti wa UVCCM
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha
Katibu wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania (B)
Wajumbe watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa - 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa - 2
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya - 1
Katibu wa Kamati ya Madiwani - 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)- 2


Mkutano wa wadau wa blog Tanzania ulivyofanyika kwa mafanikio

Disemba 05 na 06 mwaka huu 2016 ulifanyika Mkutano Mkuu wa Waendeshaji/ Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini kupitia umoja wao wa Tanzania Bloggers Network TBN, uliofanyika ukumbi wa PSPF Jijini Dar es salaam.


Siku ya kwanza ilikuwa mahususi kwa ajili ya semina kwa wanablogu hao juu ya namna ya kuendesha mitandao yao kwa ajili ya manufaa ya kijamii na yao pia. Siku ya pili ilikuwa mahususi kwa ajili ya mkutano Mkuu ambapo wajumbe wa mkutano huo waliwachagua viongozi wao ambapo Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (aliyesimama juu) na wasaidizi wake walisalia katika nafasi zao.
#BMGHabari


Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambapo alitamka rasmi kwamba serikali inatambua mchango wa wanablogu nchini katika kuipasha jamii habari hivyo itaendelea kushirikiana nao akionya watendaji wa serikali hususani maafisa habari wa mikoni wasiotoa ushirikiano kwa wanablogu hao kuacha mara moja tabia hiyo.

Katika kilele cha mkutano huo, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye, ambaye alikiri umuhimu wa wanablogu nchini akisema kwamba, watatambuliwa rasmi kupitia kanuni za sheria mpya ya vyombo vya habari nchini ya mwaka 2016 na kwamba watapewa kadi za wanahabari (Press Card) ili kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.

Sunday, December 11, 2016

Naibu Waziri Muungano atembelea Kituo cha Ujasiriamali Zanzibar

 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimksikiliza Mkurungenzi wa Kituo cha Ujasiriamali Kutengeneza Nafasi za Kibiashara kwa Vijana Zanzibar Ndg, Ameir Sheha akitowa maelezo kwa Naibu Waziri alipowasili katika viwanja vya Kituo hicho huko Mbweni Zanzibar wakati wa ziara yake Zanzibar. 
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akimsikiliza Mtaalamu Ufundi wa Kituo hicho Dr. Rajeev Aggrwal akitowa maelezo ya mafunzo kwa Vijana wanaojiunga na Kituo hicho kupata Elimu ya Ujasiriamali na baadae kujiajiri mwenyewe baada ya kupata ujenzi kupitia kituo hicho, kilioko katika majengo ya Chuo cha Karume Mbweni Zanzibar.

Rais Dr Magufuli aongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam


Picha namba 3. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Picha namba 1. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jijini Dar es Salaam. 

Wadau wazindua unga wa viazi lishe jijini Mwanza

Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) yenye makazi yake Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akizungumza kwenye uzinduzi wa Unga wa Viazi Lishe uliofanyika hii jana Jijini Mwanza. Taaisisi hiyo imekuwa ikiwaunganisha wakulima na wataalamu wa kilimo kupitia vyombo vya habari.

Unga wa viazi lishe ni muhimu kiafya kwani una wingi wa vitamini A miongoni mwa vitamini mbalimbali ambapo husaidia kuondokana na matatizo ya kuona (upofu). Pia viazi hivyo hutumika kama chakula, na unga wake ni bora kwa ajili ya utengenezaji wa mandazi, chapati, keki, biskuti na vitafunwa vya kila aina.

Taasisi hiyo imeshirikia kama miongoni mwa taasisi hususani za wajasiriamali wanawake zinazojihusisha na kilimo ikiwemo mbogamboga na matunda. Lengo lake ni kuhakikisha wanawake wanajiinua kiuchumi ili kuondokana na utegemezi na hatimaye kuondoana na adha zinazoweza kuwakumba ikiwemo ukatili kutokana na utegemezi.

Uzinduzi huo umeenda pamoja na Kilele cha Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani, yaliyoanza Novemba 25,2016 hadi jana Disemba 10,2016.

Friday, December 09, 2016

Mwamuzi wa soka Tanzania azawadiwa gari

Wadau kadhaa wa mpira wa miguu, wamemzawadia gari Jonesia Rukyaaa mwamuzi mwandamizi wa FIFA ambaye hivi karibuni alichezesha vema michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake iliyofanyika nchini Cameroon.
Jonesia, ambaye amepata pia kuchezesha mchezo wa watani wa jadi katika soka nchini miaka miwili iliyopita, alichezesha mechi ya awali na kuonekana kutokuwa na upungufu kwenye kutafsiri sheria 17 za soka, alipangwa kuchezesha mechi ya mshindi wa tatu kati ya Ghana na Afrika Kusini.

Umahiri wake, umevutia wengi wakiwamo wadau wa mpira wa miguu ambao hawakupenda kutajwa walioamua kumzawadia gari aina Toyota Vits ikiwa ni zawadi na kumbukumbu yake baada ya kuiwakilisha vema nchi.
Kwa upande wa TFF ilimtuza Mwamuzi Jonesia cheti cha kutambua uwezo na kufikia hatua ya kulitangaza shirikisho  na nchi kwa ujumla. Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi ndiye aliyemkabidhi funguo za gari Jonasia.

Wapenda gwaride jijini Dar es Salaam ‘kilio’

Na Rahim Kambi, Dar es Salaam
NI kilio kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kuwatangazia wakazi na wananchi wa jiji la Dar es Salaam kuwa sherehe za Miaka 55 ya Uhuru zinaweza kuwa za mwisho kufanyika jijini hapa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi waliojitokeza katika sherehe za miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli alisema kuwa tamko lake kwa Watanzania linakuja kutokana na kuazimia sherehe kama hizo miaka ijayo zitafanyika mkoani Dodoma ambapo serikali yake itakuwa imehamia huko ikitokea jijini Dar es Salaam.

Dr Magufuli aliyasema hayo katika Maazimisho ya Miaka 55 ya Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru na kuhudhuriwa na watu mbalimbali, ambapo majeshi ya Tanzania yalionyesha uwezo mkubwa katika kuonyesha umahiri wao.

“Naweza kusema kwamba sherehe kama hizi katika jiji la Dar es Salaam zitakuwa za mwisho kwa sababu mwaka ujao zitafanyika Makao Makuu ya nchi yetu, mjini Dodoma, hivyo tukio kama hili litakuwa rasmi kwa ajili ya kuwaaga wana Dar es Salaam,” alisema Rais Magufuli.

Mbali na kuhama kwa sherehe hizo, Rais Magufuli pia alitumia muda huo kuwapongeza Watanzania wote kwa kuazimisha miaka 55 ya Uhuru, akisema nchi imeendelea kupiga hatua kubwa ya kiuchumi, kielimu na kiutamaduni.

Aliwataka Watanzania wote kumuunga mkono yeye na serikali yake pamoja na watumishi wake ili kuhakikisha kwamba wanafanya kazi kwa nguvu zote ili kurahisisha maendeleo.


Aidha Rais Magufuli alitumia muda huo kuwaasa watu wanaoendelea kuendekeza vitendo vya rushwa na ufisadi akisema kuwa ataendelea kula nao sahani moja ili kuhakikisha kwamba nchi yake inaondokana na adha hiyo inayochelewesha maendeleo.

Thursday, December 08, 2016

Mkuu wa Mkoa wa Singida ateuliwa kuwa Katibu Mkuu Kilimo

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe pichani
Na Mathias Canal

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Gerson Msigwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jan tarehe 07 Desemba, 2016 alifanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo;



Dkt. Magufuli amemteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.
Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mhandisi Mathew Mtigumwe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Kampuni ya Bia ya Serengeti yazindua mradi wa maji Same

Mkuu wa wilaya ya same Bi Rosemary Semanyole akifurahi pamoja na baadhi ya viongozi wa serengeti breweries Limited .kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasialiano wa SBLJohn Wanyancha  mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha makanya..Hafla ya uzinduzi ilifanyika katika kijiji cha Makanya wilaya ya same mapema jana.
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

KAMPUNI ya Bia Serengeti leo imezindua  mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 83  katika eneo la Makanya wilayani Same  ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.


Ukiwa na uwezo kwa  kuhudumia watu 10,629, mradi huo unajumuisha  kisima  pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji  ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila saa moja.


Akizungumza katika  hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL, John Wanyancha  alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni mionmgoni mwa  mikakati kama hiyo  ambayo kampuni hiyo ya bia  imeiendesha  katika mikoa ya  Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha  zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.

Tamasha la Sifa za Yeriko kufanyika Dar es Salaam na Arusha



Miaka 25 ijayo, Takribani asilimia 75 ya wakazi wa Afrika Mashariki watakuwa vijana,na hii inamaanisha nguvu kazi kubwa itakuwa mikononi mwao. Lakini kama watasalia kuwa idadi kubwa basi na kuwa na maarifa ya kuendesha nchi, basi changamoto itakuwa kwa ukuaji wa nchi.

Vijana wao huona kama wana mchango katika jamii, hasa kwenye makusanyiko ya kijamii mathalani misiba, ambapo hutakiwa kuchangamkia kwenye shughuli zenye uhitaji wa nguvu. Lakini kama fursa ya uwepo wa vijana katika jamii itatumiwa vema, basi nyanja zote za maendeleo zitaendeshwa vema, na watakuwa na uwezo wa kutatuza matatizo yaliyo kwenye jamii – sawasawa na malengo endelevu namba 2 na namba 8 za umoja wa mataifa, zinazolenga kumaliza masuala ya njaa, na pia uhakika wa kazi na ukuaji wa uchumi, ikiwemo pia lengo namba 4 – kuwa na elimu bora.

Uwepo wa Tamasha la Sifa za Yeriko ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa Maono Foundation Limited na washirika wake kuwa sehemu ya kutatua matatizo haya kwa kuanzisha kituo cha ukuzaji wa vipaji kwa vijana, kusudi waweze kuwa sehemu ya suluhu ya changamoto kwenye jamii.Mkakati wa muda mfupi, ni kuhudumia moja ya kituo cha watoto yatima cha Guardian Angels House of Hope chenye uhitaji wa taaluma za watoto kukuzwa,lakini changamoto ikawa kukosekana kwa ada na mahitaji mengine ya shuleni.Kwa kujumuika kwenye tamasha hili, si tu kwamba watakuwa wanamuaibisha mwovu shetani kwa kuangusha ngome zinazowasumbua kwenye Nyanja mbalimbali maishani, bali pia watakuwa wamechangia katika kutimia kwa malengo ya Maono Foundation.

Wednesday, December 07, 2016

Wahariri wakutana kujadiliana juu ya tasnia ya Habari

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wahariri  kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari uliyopitishwa na Bunge pamoja na kujadili mpango mkakati wa TEF wa kuendeleza tasnia ya habari nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
WAHARIRI wa vyombo vya habari wamekutana katika mkutano maalumu wa siku mbili kwa ajili ya kujadili mambo kadhaa yanayohusu tasnia hiyo nchini.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga alisema mkutano huo utawajumuisha wadau wa sekta ya habari kutoka ndani na nje ya nchi.

"Tumewaalika wenzetu wa nje ili watupe uzoefu wa jinsi wanavyofanya katika tasnia ya habari katika nchi zao," alisema Makunga.


Taasisi ya African Relief yaanzisha kilimo cha umwagiliaji Rufiji

Mkurugenzi wa Taasisi ya African Relief Organization, Samy  Mohammed Elazeb (kulia) akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.Picha zote na Richard Mwaikenda
  Mwenyekiti wa Taasisi ya African Relief Organization, Abdallah Ndauka akisimamia trekta likilima shamba lenye ukubwa wa ekali 2500 eneo la Khanga, katika Kijiji cha Chumbi C, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani mwishoni mwa wiki.Taasisi hiyo itaanza uzalishaji wa mazao ya mahindi na mpunga.

Wachezaji wa Golf JWTZ wapewa somo

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Wachezaji wa Golf wa klabu ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wametakiwa kutobweteka na mfululizo wa ushindi waliopata katika mashindano mbalimbali badala yake wemewatakiwa kujiweka tayari na mashindano ya Kimataifa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa klabu  hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo mara baada ya kurejea kwa Timu hiyo iliyokuwa ikishiriki Mashindano ya Chairman Troph yaliyofanyika kwa siku Mbili Moshi Mkoani Kilimanjaro ambako ilinyakua vikombe Vinne.
“Najua sie ni Klabu bora ya Golf nchini na yenye wachezaji wazuri kitaifa lakini sasa ni wakati wa kujiandaa Kimataifa ambako tutaitangaza nchi vyema katika mchezo huo na kuliletea Sifa jeshi letu.” Alisema Brigedia Jenerali  Luwongo.

Aliongeza kuwa licha ya kuweka maandalizi ya ushiriki wa kimataifa kwa mwaka 2017 lakini ni fursa kwa wanaotaka kujifunza golf wakati huu wa likizo za mwisho wa mwaka kujitokeza klwani shughuli zote za golf katika uwanja wa Lugalo zitaendelea  kama kawaida.
Kwa Upande wake  mkuu wa Utawala wa Klabu ya Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule alisema katika mashindano hayo ya siku mbili yaliyofanyika Desemba Tatu na Nne Mwaka huu huku  yakitumia mtindo wa Stroke Play Net ambapo Timu ya Lugalo iliwakilishwa na wachezaji 10  Kapteni  Mandengule Alisema  walifanikiwa kunyakua vikombe vitano ambavyo vimedhihirisha kuwa umahiri wa klabu unazidi kuongezeka kwani ni mashindano manne mfululizo Timu ya Lugalo inafanya vyema.

Alisema kutoka  Klabu ya Lugalo mshindi wa Kwanza ambaye alifanikiwa kuleta ushindi wa Jumla  kwa klabu ya Lugalo ni Seif Mcharo Divisheni  A  Mshindi ni Richard Mtweve, Divisheni  C ilichukuliwa na Enock Magile na Wanawake mshindi wa kwanza ni Vicky Elias na Mshindi wa pili ni Sara Denis. Kwa Upande wake   Mshindi wa Jumla kutoka Lugalo Seif Mcharo alisema Ushindio huo ulitokana na maandlizi mazuri yaliyofanyika wakati wa kuelekea katika mashindano mbalimbali ambayo yamekuwa yakiandaliwa.

Kwa  upande wake mshindi wa Divisheni A Richard Mtweve alisema licha ya Kuibuka na ushindi lakini ushindani ulikuwa mkubwa kutokana na matokeo mazuri yaliyotokea kwa wachezaji wote kupata alama nzuri kulinganisha na Alama zilizopatikana katika mashindano mengine. Katika mashindano hayo Klabu Tano zilishiriki katika mashindano hayo ambazo ni Lugalo, Gymkhana Dar es Salaam , TPC, KILI,MOSHI.

MGODI UNAOTEMBEA: Nina hamu ya kuiona CCM ya Dr Magufuli

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
NAAM! Macho na masikio ya wengi katika nchi yetu kwa sasa ni namna gani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaingia kwenye mabadiliko makubwa kutokana na aina ya utendaji wa Mwenyekiti wake, Dr John Pombe Magufuli.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dr John Pombe Magufuli, pichani.

Dr Magufuli ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anajulikana kama kiongozi asiyependa ujinga na mtumbua majipu, aliyerithi mikoba ya Uenyekiti wa CCM Taifa kutoka kwa Mwenyekiti Mstaafu, Dr Jakaya Mrisho Kikwete. 

Dr Kikwete alikuwa mwenyekiti wa CCM Taifa huku akitawaliwa na huruma, tabasamu kiasi cha watendaji wake kutumia mwanya huo kuwa wala rushwa, wachumia tumbo na ‘majipu’ yanayostahili kutumbuliwa bila ganzi. Ndio ni majipu. Tena majipu makubwa kuliko hata yale ya watendaji wa serikali, ukizingatia kuwa kushamiri kwao wengi wao wamezalishwa na kuchochewa na mfumo mbovu wa upatikanaji wa viongozi wa CCM kwa miaka ya hivi karibuni.
Dr Magufuli akiwasalimia wajumbe wa CCM.
Hakuna asiyefahamu majipu hayo. Hata alipokuwa anahutubia wajumbe mjini Dodoma wakati anakabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa CCM Taifa, Dr Magufuli alilizungumzia kwa kina, akionyeshwa kukerwa na aina watendaji na mfumo wa chama chake. Mwenyekiti huyo alifahamu kati ya matatizo mengi ya kupata viongozi wasiokuwa wasafi, wala rushwa, wasiokuwa na uchungu na Taifa lao, baadhi yao wanatokea kwenye chama chake.

Naye ni muathirika mkubwa baada ya kupata wakati mgumu katika mchakato wa kuomba wadhamini alipochukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama cheke kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia CCM, huku baadhi ya makada wake wakituhumiwa kumwaga fedha kama njugu ili kuongeza ushawishi kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama katika vijiji, kata, wilaya na mikoa mbalimbali ya nchi yetu.

Licha ya ukongwe wake, CCM ilianza kupoteza sifa na imani kwa wananchi wengi wa mijini huku wa vijijini nao wakianza kuangalia uwezekano wa kuongozwa na wapinzani. Wakaiona CCM ni chama cha mafisadi, wala rushwa na watoa rushwa.

Viongozi wakaanza kupatikana kwa ukwasi wa fedha. Nafasi zote za uongozi ndani ya CCM na zile za ubunge na udiwani ziliuzwa kwa fedha nyingi. Walalahoi wachache walipita. Tena kwa kufanya kazi ya ziada ama kulazimika kuwa kwenye mtandao wa wenye nazo. Kuweka mamilioni ya fedha ili kuongeza ushawishi wa kupata madaraka ndani ya CCM kilikuwa mazoea. Na kila mtu alijua hilo. Mgombea anaulizwa, “Mzee unatuachaje”?

Mpango wa huduma maalum kwa wateja wakubwa sekta ya afya wazinduliwa

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam leo asubuhi.
Kikosi kazi cha SMO. kutoka kushoto ni Benjamin Mtesigwa, Frankie Nkone, Naomi Shangali, Marko Masala na kiongozi wao, Cosmas Nalimi.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

BOHARI  ya dawa (MSD) imezindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wake wakubwa, kama moja ya hatua za kuboresha huduma kwa wateja. 
Mpango huo utawawezesha wateja hao kupata huduma ya haraka zaidi pindi wanapokuwa wanahitaji mahitaji yao.



Wateja hao ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hosipitali ya Sekoutoure Mwanza, Hospitali ya Kibong’oto, Mirembe, Hosipitali za Amana, Temeke, Mwananyamala, KCMC, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Serikali yaipigia chapuo tasnia ya blog Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni, Nape Nauye, amesema siri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingia madarakani ni mitandao ya kijamii.

Akifunga kongamano la mkutano mkuu wa Umoja wa Wanachama wa mitandao ya kijamii (blogeers), Nape alisema CC imeingia madarakani baada ya kuandikwa kwa upana mkubwa katika mitandao ya kijamii.

Alisema mitandao ya kijamii iko na nafasi kubwa katika jamii ambapo asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia mitandao ya kijamii ambapo habari nyingi wakati wa kampeni walikuwa wakisoma katika mitandao hiyo.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...