https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, April 24, 2016

Pigo: Gwiji wa muziki wa rhumba duniani, Papa Wemba afariki Dunia

Majonzi: Mwanamuziki maarufu anayejulikana kama Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba ama "Papa Wemba", wa nchini Kongo na muziki wake unaojulikana sehemu nyingi za Afrika na Dunia kwa ujumla, amefariki Dunia. Mwanamuziki huyo amefariki huku akiwa na miaka 66. Kifo cha gwiji huyo wa muziki wa dansi wa asili ni pigo kwa wadau, mashabiki wa muziki wa dansi.
Marehemu Papa Wemba, pichani enzi za uhai wake.

Friday, April 22, 2016

Wananchi wa jimbo la Handeni wamlilia Waziri wa Maji

Na Mwandishi Wetu, Tanga
WAZIRI  wa maji  Mhandisi  Gerson Lwenge, pichani juu ameombwa  kuingilia kati  na  kushughulikia  kwa haraka  utata  uliogubika  utekelezaji  wa mradi  wa  Bwawa  la maji  la malezi  lilipo kata  ya Malezi ,Mjini Handeni  ambao  haujaanza  licha  ya Benk ya Dunia  kutoa shs. Milioni 700  kwa  ajili  ya mradi huo.
Wakizungumza katika mahojiano na wawakilishi wa vyombo vya habari waliokuwa wanafuatilia utekelezaji wa mradi huo, wakazi hao ambao wanalazimika kutembea kilometa zaidi ya 5 kufuatilia maji  katika vyanzo vya maji wamesema hawaoni sababu ya mradi huo kutokuanza licha ya fedha hizo kutolewa.
Kitombo alisema kwa taarifa alizonazo mwaka 2013 Benki ya Dunia iliingiza sh. Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo ambao  unatarajiwa  uwanufaishe Wakazi Zaidi  ya 6000. Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni sh. Milioni 880. 
Aliendelea kueleza kuwa mwaka jana sh. Milioni 300 zilliingizwa katika akaunti na kufanya jumla ya fedha zilizoingizwa katika akaunti ni shs. Milioni 700
Pia alieleza mshangao wake kwa nini mradi huo bado unaendelea kutekelezwa na Halmshauri ya Wilaya wakati ambapo eneo la mradi liko Halmashauri ya Mji.

Monday, April 18, 2016

Habibu Foundation yaadhimisha siku yao kwa kutoa misaada wilayani Mwanga

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation, Juma Mndeme, mwenye miwani akizungumza jambo baada ya kumaliza kukabidhi misaada ya mabenchi ya kukalia, sabuni na vinywaji kwa Kituo cha afya Mwanga, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro. Aliyeshika majaketi ni Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo hicho Honest Temba na aliyeshika simu ni Meneja Uhusiano wa Habibu Foundation, Julysiza Mangiseni.

Na Mwandishi Wetu, Mwanga
MAADHIMISHO ya Siku Maalum ya Habibu Day wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro yamefanyika kwa mafanikio kwa kushirikisha matukio mbalimbali yakiwamo ya kutoa misaada katika kituo cha Afya Mwanga, kutoa misaada jeshi la Polisi, pamoja na kufanyika mijadala mbalimbali ya kielimu iliyoendeshwa na wanafunzi wa shule za sekondari wilayani humo.

Katika muda wa mijadala, wanafunzi hao walitumia muda mwingi kuzungumzia mfumo wa kielimu nchini Tanzania sanjari na upangaji wa matokeo ya mitihani kutoka Division na GPA iliyoondolewa rasmi katika mfumo huo nchini hapa, huku mgeni rasmi akiwa ni Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Jomo Kenyata kilichopo Arusha, Profesa Ward Mavura.

 Meneja Uhusiano wa Taasisi ya Elimu ya Green Bird Education Institute & Habibu Foundation, Julysiza Mangiseni, akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo yaliyoanzia kutoa zawadi mbalimbali. 

Awali ratiba ilianza rasmi saa 12 asubuhi kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Green Bird Girls, Green Bird Boys, Green Bird Collage zinazomilikiwa na taasisi ya Habibu Foundation kutembelea katika maeneo ya Ofisi ya polisi Mwanga na kituo cha afya Mwanga, pamoja na kutoa misaada kama vile mabechi ya kukalia wagonjwa, sabuni, vinywaji pamoja na vifaa ya ofisi kwa jeshi la Polisi Mwanga.

Mbunge wa Mkuranga akabidhi vifaa vya michezo kwa shule za sekondari


Na David John, Mkuranga.

MBUNGE wa Jumbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega amekabidhi jezi seti20 na mipira 20 zenye thamani ya sh.milioni 4katika shule zote za Sekondari zilizopo katika Jimboni hapa.

Akikabidhi jezi hizo wilayani hapa jana katika hafla fupi iliyowakutanisha walimu wakuu,wanamichezo,watendaji wa halmashauri ,pamoja na Ofisa Elimu ,Ulega amesema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.

"Ndugu zangu walimu na manahodha wa timu zote Kutoka shule 20 za sekondari zilizoponda ndani ya Jumbo langu la Mkuranga nimetoa vifaa hivi ili muweze kushiriki vyema katika michezo ya shule za Sekondari UMISETA nakutuletea mafanikio,"alisem Ulega.

Pia amesema kuwa anatambua kuwa kuna changamoto za kutosha katika michezo hususani vifaa vya michezo Kwa kutambua hilo ameamua kutoa vifaa hivyo huku akiwataka wanafunzi na walimu hao kusimamia vyema.

Aidha Mbunge Ulega amehaidi kutoa ushirikiano wa dhati Kwa walimu na viongozi mbalimbali wa halmashauri hiyo ili Kwa pamoja kuharakisha maendeleo jimboni hapa ikiwamo michezo.Pia amewaambia viongozi hao kujenga mashirikiano ya Katibu na yeye kama mwakilishi wao yupo tayari Kwa wakati wowote kutumika na kusikiliza maoni yao.

Kwaupande wake Ofisa Elimu wa Halmashauri Kwa upande wa shule za Sekondari Benjamini Majoya akizungumza katika hafla hiyo alisema kuwa Mbunge Ulega amefanya jambo ambalo halijawahi kufanywa Kwa viongozi wengine waliotangulia.Amesema kuwa watamuunga mkono Mbunge huyo Kwa kuhakikisha wanafanya vizuri katika nyanja ya Elimu na michezo Kwa ujumla.

"Kwanza tunashukuru Kwa vifaa hivi kwani vimekuja katika wakati muhimu ambapo tunakwenda katika mashindano ya UMISETA na Kwa vifaa hivi ushindi upo,"amesema Majoya.Pia ameongeza kuwa hakuna ubishi kwamba michezo ni ajira hivyo lazima watahakikisha vijana hao wanafanya vizuri katika michezo na taaluma pia.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...