https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, January 28, 2016

Picha mbalimbali zinazoonyesha athari ya mvua jijini Dar es Salaam

 Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha leo.
 Kituo cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa maji hivyo  kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.

Pitia tamko lote la Chama cha CUF kususia Uchaguzi wa marudiano visiwani Zanzibar

IMG-20160128-WA0019
AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.
Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

Wakabidhiwa jengo la mafunzo na madawati Kilombero

 Mwakilishi wa jamii ya wafanyakazi kutoka Afrika Kusini katika kampuni ya Illovo Tanzania (SATZ) Cathryn Morris akikata utepe wakati wa kukabidhi  jengo ambalo ujenzi wake umefadhiliwa na taasisi za (SATZ) waliotoa  5.5, Jenga Women Group milioni 4. Hafla ya kukabidhi ilifanyika Kilombero jana. Jengo hilo litatumika kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. 
 Mweka hazina wa kikundi cha Jenga cha Kilombero Candice Roe-Scott akiongea na vikundi ambavyo watafaidika na jengo jipya litakalo tumika kwa kwa ajili ya maktaba, kuwashauri yatima na watoto washio katika mazingira magumu. Jengo hilo lilikabidhiwa kwa vikundi vya kijamii jana, Kilombero

Mtandao wa Kenya umetoa uongo wa Rais Magufuli kutembelea Kenya

Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii. 
Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanhabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na  ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko waTanzania wenyewe. 
Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo! 
Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

Sunday, January 24, 2016

Rais John Pombe Magufuli atunuku Kamisheni Maafisa wapya Monduli

 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao. 
 Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono wananchi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa jeshi kwa cheo cha Luteni Usu.

Friday, January 22, 2016

Waziri Ummy Mwalimu azindua duka la dawa la MSD jiji Mwanza

 WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu (kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza jana ambalo liko ndani ya Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD, Profesa Idrisa Mtulia.

Nyota wa kikapu wa Malawi kuzikabili timu za Da

 Mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi. Wa kwanza kulia waliokaa ni mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo, wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
 Mkurugenzi wa ufundi chama cha mpira wa kikapu Malawi Obed Nyirongo  kiongeana waandishi wa  wa habari leo jijini Dar-es- Salaam kuhusu  mechi za kirafiki zitakazochezwa Jumamosi na Jumapili katika uwanja wa BBK Park na timu kutoka Malawi wa Sprite BBall Kitaa. Wa kwanza kushoto waliokaa ni mratibu wa Sprite BBall Kitaa Karabani Karabani na wengine ni wachezaji wa timu ya Bricks na Brave Hearts.
*************************
Miamba miwili ya mpira wa kikapu kutoka nchini Malawi imewasili jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya mfululizo wa mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya timu za bigwigs Jogoo, East Zone One, Mbezi na West Zone Three. Mechi hizo zenye hamasa ya aina yake zitachezwa kwenye uwanja Bball Kitaa Park, karibu na Ukumbi wa Gymkhana.
Kulingana na ratiba iliyotolewa na mratibu wa Bball Kitaa Karabani Karabani pazia la michezo hiyo litafunguliwa kesho ambapo East Zone One watakipiga na Bricks, mchezo unaotabiriwa kuwa ni mgumu na wa kusisimua. Siku hiyo hiyo Mbezi watacheza na Associate Team, mchezo ambao pia unatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Michezo hiyo bado itaendelea kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambapo West Zone Three watapambana na Bricks kabla ya Jogoo kuwakaribisha Associate team. “Tuna furaha kubwa kuandaa michezo hii ya kirafiki. Ni moja ya sehemu muhimu katika kudumisha mahusiano, vile vile kuendeleza vipaji vinavyochipukia”, Karabani alisema.

Ujio wa Bricks na Associate teams jijini Dar es Salaam imeonekana si jambo geni baada ya timu za East Zone One na West Zone Three kwenda Malawi mwaka jana. Zikiwa nchini humo, timu hizo zilishinda mechi zao kadhaa.

Friday, January 15, 2016

Esther Bulaya na Steven Wasira wapepetana Bunda

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili kuchuana vikali kwa muda mrefu. 

Waleta maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Madai hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.

Wednesday, January 13, 2016

Mbunge wa jimbo la Arumeru ajichimbia China kusaka

Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa katika moja ya karakana ya kutengeneza vifaa tiba katika mji wa Guangzhou nchini China.

Wateja wa Tigo Pesa kuvuna 4.4bn/- gawio la robo mwaka

Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao Tigo, Obedi Laiser akielezea kuhusu gawio la mwaka huu  kwa watumiaji wa Tigo Pesa, kushoto kwake ni Meneja wa Mawasiliano, John Wanyancha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kampuni inayongoza katika kuleta maisha ya kidijitali kwa jamii, Tigo, imetangaza tena malipo ya robo mwaka ya shilingi bilioni 4.4 (dola milioni 2.1) kwa watumiaji wake wa huduma ya Tigo Pesa wapatao milioni 4.6. 

“Gawio hili la faida linalipwa kwa watumiaji wote wa Tigo Pesa wakiwemo wateja binafsi, mawakala wa rejareja na washirika wetu wa kibiashara, kila mmoja kutokana na thamani  ya fedha aliyojiwekea katika akaunti yake ya Tigo Pesa,” alisema Mkuu wa Fedha na Tahadhari wa Huduma ya Fedha kwa njia ya mtandao, Obedi Laiser.

 Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Laiser amesema  kuwa hii itakuwa ni mara ya kwanza Tigo kuwalipa gawio la faida watumiaji wa Tigo Pesa kwa mwaka wa 2016  akibainisha kuwa malipo hayo ni faida inayopatikana kutokana na amana ya mfuko wa Tigo Pesa uliyowekezwa katika benki za kibiashara hapa nchini. 

Akamatwa na meno ya tembo kilo 50 mkoani Katavi

Meno ya Tembo vipande 8 vyenye uzito wa kilo 50 ya thamani  ya milioni  120  ambayo ni sawa na Tembo hai wane aliyokamatwa nayo hivi karibuni mtuhumiwa  Nzuri Ndizu Mkazi wa Kijiji cha Mbede Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. 

Picha  na  Walter Mguluchuma, Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika  kwa jina la  Nzuri  Ndizu (44) Mkazi wa Kijiji cha Mbede  Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi  amekamatwa akiwa  na meno  ya Tembo  nane  yenye uzito wa kilogramu 50 yakiwa na thamani ya shilingi milioni 120 ambapo ni sawa na Tembo wanne waliuwawa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari aliwaambia waandishi wa Habari   kuwa  mtuhumiwa huyo alikamatwa   mida ya saa tatu  na nusu .
Kidavashari alisema mtuhumiwa  Ndizu  alikamatwa  kufuatia   misako  na  uparesheni mbalimbali zinazoendelea kufanywa  na Jeshi la Polisi  ikiwa ni kuhakikisha  wahalifu  wa makosa mbalimbali wakimemo  wawindaji  haramu  wa wanyama pori  wanakamatwa.
Mtuhumiwa  Nzuri  Ndizu,  Mkazi wa Kijiji  cha Mbende Wilaya ya Mlele, akiwa katika  ofisi ya Kamanda  wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  baada ya kukamatwa na meno ya Tembo  vipande  nane   yenye thamani ya shilingi  milioni  120  hapo juzi.

Umoja wa Makanisa wafanya maombi mazito Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza

Umoja wa Makanisa Jijini Mwanza unawakutanisha Watanzania katika Uwanja wa Furahisha uliopo katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa ajili ya Maombi ya rasmi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na Wasaidizi wake ili kuliongoza Taifa vema.

Pia maombi hayo ni mahususi kwa ajili ya kuliombea Taifa kwa ajili ya kupata baraka mbalimbali. Kuanzia majira ya saa saba Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameanza kujongea kwa ajili ya kujumuika pamoja katika maombi hayo ambayo yatafikia tamati jioni.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo huku wageni mbalimbali wakiwemo Viongozi wa dini pamoja na waimbaji nyimbo za injili wakihudhuria katika maombi hayo.

Tuesday, January 12, 2016

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto akagua jengo la Zahanati kijijini Mpingi


Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi.
Na Mwandishi Wetu, Songea
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la Zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo. 

Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa  Bima ya Afya.

Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.

Kamati ya Uendeshaji wa ligi waipa kicheko Polisi Dodoma Ligi Daraja la kwanza

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi umeipa Polisi Dodoma ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Mji Mkuu FC kumchezesha mchezaji Peter Ngowi aliyekuwa na kadi tatu za njano kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Desemba 26, 2015 mjini Dodoma.
Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(4) na 14(37) ya Ligi Daraja la Kwanza. Mji Mkuu FC ilikuwa imeshinda mabao 2-1 katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa.
Kamishna wa mechi ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Polisi Tabora na Panone FC ya Moshi, Shabani Funyenge amesimamishwa kutokana na ripoti yake ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kuwa na upungufu.
Klabu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu yake kutoa kashfa na lugha za matusi wakati wa mechi ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Kiluvya United iliyofanyika Novemba 8, 2015 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Kaume jijini Dar es Salaam.
Pia imetakiwa kulipa kibendera cha kona (corner flag) pamoja ubao wa matangazo wa geti la kuingilia ndani kwenye Uwanja wa Karume ambavyo vilivunjwa na washabiki wa timu hiyo mara baada ya mechi hiyo.
Mtunza vifaa wa timu ya Kimondo, Emily Nehemia, Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Idd Kibwana, Kiongozi wa Panone FC, Said watafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.

Serikali yatoa taarifa kwa umma juu ya mwelekeo wa ugonjwa Kipindupindu

DSC_0063
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dkt. Rufaro Chatora

Taarifa kwa umma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu hapa nchini ni kama ifuatavyo; Tangu ugonjwa huu uanze, jumla ya watu 13,491 wameugua Kipindupindu, na kati yao jumla ya watu 205 wameshafariki kwa ugonjwa huu. Katika kipindi cha wiki iliyoanza tarehe 04 hadi 10 Januari 2016, kumekuwa na jumla ya wagonjwa 615 walioripotiwa nchini kote na vifo vitatu (3). Mikoa ambayo bado imeripoti kuwa na ugonjwa huu ndani ya wiki moja iliyopita ni 11 kati ya 21 iliyokuwa imeripoti ugonjwa hapa nchini. Mikoa hiyo ni pamoja na Morogoro, Arusha, Singida, Manyara, Pwani, Dodoma, Geita, Mara, Tanga, Mwanza na Simiyu. Kati ya hiyo, mikoa inayoongoza kwa kuripoti idadi kubwa ya wagonjwa wapya ndani ya wiki moja iliyopita ni pamoja na Morogoro (Manispaa ya Morogoro 87, Halmashauri ya Morogoro 66), ukifuatiwa na Arusha (Arusha Manispaa 50), Singida (Iramba 40) na Manispaa ya Dodoma ( 33).

Aidha, mikoa iliyokuwa na maambukizi lakini kwa muda wa wiki moja iliyopita hakukuwa na mgonjwa yoyote wa kipindupindu ni pamoja na Mbeya, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera, Lindi. Vile vile mkoa wa Dar es Salaam ambako ndiko ugonjwa ulianzia na kudumu kwa muda wa miezi minne (4) haujaripoti mgonjwa wa kipindupindu kuanzia tarehe 22/12/2015. Mikoa ambayo ilikwisha kuwa na ugonjwa huo lakini hapajakuwepo na wagonjwa wowote kwa muda wa zaidi ya miezi miwili iliyopita ni pamoja na Shinyanga, Kilimanjaro na Iringa. Pia mikoa ambayo haijawahi kutoa taarifa ya ugonjwa wa kindupindu tangu mlipuko huu uanze hapa nchini ni Njombe, Ruvuma na Mtwara.

Monday, January 11, 2016

Rais Magufuli amtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye Muhimbili kumjulia hali


 
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS



 Na Mwandishi Wetu

BONDIA Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebela, January 30 katika Ukumbi wa Sativa uliopo Kyela, mkoani Mbeya, mpambano huo wa raundi nane wa uzito wa juu utafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa huo

Akisaini mkataba huo mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa, amesema ata akikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito huo

Wizara ya Maji na Umwagiliaji waimwagia sifa DAWAS

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (DAWASCO) Mhakndisi Cypian Luhemeja akiongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Mfutakamba, wakielekea katika kikao cha uongozi na wafanyakazi wa DAWASCO kilichofanyika makao makuu ya shirika hilo. 
Mkurugenzi wa Rasilimali watu w Shirika la Maji safi na Maji taka Dar es Salaam,DAWASCO,Bi,Joy Chidosa akifanya utamburisho katika kikao hicho.

Sunday, January 10, 2016

Mbwana Samatta, alistahili, anastahili na atastahili pia, HONGERA

Nyakati fulani nilipokuwa Msemaji Mkuu wa klabu ya African Lyon, tuliweka kituo chetu Morogoro Mjini wakati tunaelekea Turiani, mkoani Morogoro kucheza na timu ya Mtibwa Sugar. Tuliingia Mjini Morogoro jioni na kufikia tulipopangiwa. Baada ya kushukuru kwa kufika salama Morogoro, 
Mbwana Samatta, pichani
Kocha Mkuu Charles Boniface Mkwassa, akatoa neno kwa msafara mzima na wachezaji wake, akiwamo nyota wetu Mbwana Samatta. Namsema ni nyota kwa sababu tangu wakati huo tulikuwa tunategemea uwezo wake, akishirikiana na nyota wengine kwa ajili ya kupata ushindi. Mkwassa akasema, " Jamani sisi wote ni watu wazima, hivyo sioni sababu ya kuanza kuchungana chungana. Lazima wachezaji mjue nidhamu, kujituma ndio njia ya kufika mbali katika sekta ya mpira wa miguu. 

Hivyo natumaini kila mtu anajua kilichotuleta Morogoro kwa ajili ya kwenda kucheza na Mtibwa Sugar. Hakuna wa kuwachunga," Mwisho wa kunukuu. Kisha watu wakachanguka. Lakini dakika 20 zilipotimu, nikamuona Samatta anaingia kwenye room yake, mimi nilikuwa nimekaa mapokezi, nasubiri wachezaji wangu warudi ndani, huku nikiangalia tv na kubadilishana mawazo tuliokuwa hapo. 

Saturday, January 09, 2016

Mbwana Samatta arejea Tanzania usiku wa manane, TFF wapongeza wadau wa soka

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limewashukuru watanzania wote, wapenzi, na wadau wa mpira wa miguu Tanzania waliojitokeza usiku saa 8 uwanja wa ndege wa JK Nyerere kumpokea mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani Mbwana Samatta.
Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa JK Nyerere, Samatta alipokelewa na viongozi wa serikali, TFF, familia yake wakiwemo baba na mama yake mzazi na watanzania wengi walijitokeza kumlaki mchezaji huyo.
Mara baada ya mapokezi ya uwanja wa ndege, TFF ilimpeleka moja kwa moja kupumzika katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta jijini Dar es salaam, ambapo imemlipia gharama ya kukaa kwa siku mbili.
Akiwa hoteli ya Serena, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mama Juliana Yassoda alitoa salamu za pongezi kwa niaba ya Serikali, kisha mchezaji alipata nafasi ya kuongea na waandishi wa habari.
Kwa kuwa Jumanne, Januari 12 ni Sikukuu ya Mapinduzi, na Janauri 13 ni fainali ya kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar, siku ya Alhamisi Januari 14 TFF imeandaa dua maalumu ya kumpongeza Samatta itakayongozwa na viongozi wa dini mbalimbali katika uwanja wa Karume kuanzia saa 11 jioni.
Hata hivyo ratiba zingine za kumpongeza Mbwana Samatta zinazoweza kuandaliwa na wadau wengine zinaweza kuendelea ilimradi TFF ijulishwe mapema kwa ajili ya kuratibu uwepo wa mchezaji mwenyewe.

Kituo cha Alafa wilayani Temeke watoa huduma za afya Darul Arqam Childrens Home Tandika

Muhudumu wa Afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha Alafa kilichopo wilaya ya Temeke Bi, Latifa Masasi kushoto akichukua vipimo vya damu ya mtoto Raban Mansur wakati alipotembelea Kituo cha watoto yatima cha Darul-Arqam Childrens Home kilichopo Tandika Magorofani kwa ajili ya kuwapima afya watoto wanao lelewa katika kituo hicho
Muhudumu wa Afya ya baba mama na mtoto wa kituo cha alafa kilichopo wilaya ta Temeke Bi, Latifa Masasi kushoto akichukua vipimo vya damu kwa mtoto Abdulatif Said kwa ajili ya kujua afya yake kushoto ni Hamis Rajabu wakati alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Darul-Arqam Childrens Home kilichopo tandika magorofani kwa ajili ya kuwapima afya watoto wanao lelewa katika kituo hicho

Friday, January 08, 2016

Mbwana Samatta aiweka kileleni Tanzania kwa tuzo ya mwanasoka bora

Na Mwandishi Wetu, Nigeria
NYOTA wa kusukuma kabumbu wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Kongo kwenye klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta, usiku wa kuamkia leo, Abuja nchini Nigeria, ameibuka na tuzo ya mchezaji bora kwa wachezaji wanaocheza Barani Afrika.
Mbwana Samatta, akiwa uwanjani kwenye timu yake ya TP Mazembe.
Tuzo hiyo inazidi kumuweka katika nafasi nzuri mchezaji huyo aliyeibukia katika timu ya Mbagala Malket, African Lyon, Simba SC na sasa TP Mazembe. Watanzania wengi wamekuwa wakielezea hatua hiyo kama sehemu ya kuonyesha furaha yao kutokana na kijana huyo mdogo kuiweka nchi katika kilele cha mafanikio.


Samatta alitangaza saa chache kabla ya fainali hizo kuanza, kuwa ana uhakika mkubwa wa kushinda kwenye tuzo hizo kutokan na nafasi yake nzuri ya kucheza akiwa kwenye klabu yake ya TP Mazembe.

Tuesday, January 05, 2016

Waziri wa Maliasili Prof Maghembe asimsimamisha kazi kigogo wa misitu na maofisa wote wa misimu wa mikoa

Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika kikao na Idara ya Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Januari, 2015. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Meja Jenerali Gaudence Milanzi.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi Endelevu ya Rasilimali za Misitu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Bw. Mohammed Kilongo na Maofisa wa Misitu wa Mikoa nchi nzima kupisha uchunguzi wa upotevu wa mapato ya Serikali.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia) akizungumza katika kikao na Idara ya Misitu na Nyuki pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo tarehe 05 Januari, 2015.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya Wizara hiyo Dar es Salaam, Prof. Maghembe amesema agizo hilo limekuja kutokana na ubadhilifu unaofanywa na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri ya Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Ameagiza pia maofisa hao wote wanaokusanya maduhuri ya Serikali katika Wilaya watumie muda wa siku kumi kuanzia leo kuhakikisha maduhuri yote yaliyokusanywa yanapelekwa benki ikiwa ni pamoja na kukabidhi vitabu vya kukusanyia mapato kinyume cha hapo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Rais Dr John Magufuli apokea hati za utambulisho za mabalozi watatu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo 05 Januari, 2016 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, tukio ambalo limefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.

Mabalozi ambao wamekabidhi hati zao za utambulisho ni Balozi wa Jamhuri ya Korea Mheshimiwa Song Geum-young, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) Mheshimiwa Roeland Van de Greer na Balozi wa Palestina Mheshimiwa Hazem M. Shabat.

Akizungumza na mabalozi hao kwa nyakati tofauti, Rais Magufuli amewapongeza kwa kuteuliwa kuja kuziwakilisha nchi zao hapa nchini, na amewaahidi kuwa serikali yake itatoa ushirikiano kwao ili shughuli zao ziweze kufanikiwa. 

Aidha, Rais Magufuli amesema Tanzania inatambua matokeo ya ushirikiano wa kimaendeleo kati ya nchi hizo na amewahakikishia mabalozi hao kuwa ushirikiano huo utaendelezwa kwa manufaa ya wananchi.

Kwa upande wao Mabalozi waliokabidhi hati zao za utambulisho wamempongeza Rais Magufuli kwa uongozi mzuri alioanza nao tangu aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wamemuahidi kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano hususani katika shughuli za maendeleo
©Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
05 Januari, 2016

Dk Kigwangalla atembelea Hospitali ya Muhimbili na kukagua mashine ya CT-Scan

IMG_0833
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016. Picha zote na Zainul Mzige.

Na Rabi Hume, Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi. Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la dawa la MSD na kukagua ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI. Akizungumzia ziara hiyo mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa ili kuweza kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika hospitali hiyo ya taifa tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo hali iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali.
IMG_0836
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akitoka katika ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

Dk. Kingwangalla alisema amefurahishwa na utoaji wa huduma katika upimaji kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI ambazo awali wakati wanaingia madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya ufanyaji wa kazi na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuifanya hospitali hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa hospitali ya taifa. Alisema limekuwa jambo ambalo linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika hospitali ya taifa zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali za watu binafsi na akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa Muhimbili kuwa hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi wananchi wenye uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda hospitalini hapo.

Monday, January 04, 2016

Karimjee yakabidhi scholsrship kwa washindi wa sayansi

Wanafunzi John Method (kushoto) na Edwin Luguku (wa pili kulia) kutoka Shule ya Sekondari Mzumbe mkoani Morogoro wakipokea hati zao za ufadhili kutoka kwa Karimjee na Ofisa Ubalozi wa Ireland nchini, Bi. Carlo. Wanafunzi hao waliibuka washindi wa jumla katika maonesho ya Sayansi kwa Shule za Sekondari mwaka 2015 yanayoandaliwa na taasisi ya Young Scientists Tanzania (YST). Picha zote na Daniel Mbega.

Tuwajali Foundation watembelea kituo cha Sifa na kutoa misaada

Baadhi ya wana kikundi cha Tuwajali Foundation wakiwa pamoja na watoto wa kituo cha Sifa wakati walipo watembelea na kutoa msaada.

Baadhi ya vitu vimetolewa kwa kituo cha Sifa Foundation.

Sunday, January 03, 2016

Bondia Francis Cheka kukwaana na Ajetovic Februari 27

Promota Juma Msangi kushoto akiwa na Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' na Meneja msaidizi wa bondia  Faransic Cheka  wakitambulisha mpambano wa bondia Cheka wa Tanzania, dhidi ya Muingereza, Ajetovic, mbele ya waandishi wa habari mpambano utakaofanyika februari 27 katika Uwanja wa Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Picha zote na SUPER D.
 Promota Juma Msangi kushoto akiwa na Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' na Meneja msaidizi wa bondia  Faransic Cheka  wakitambulisha mpambano wa bondia huyo mbele ya waandishi wa habari. Pambano hilo litafanyika Februari 27 katika Uwanja wa Leaders Club, jijini Dar es Salaam.

Nevy Kenzo wamtimulia vumbi Diamond chat za MTV Base

Kundi la mziki la Navy Kenzo linaloundwa na Aika na Nahreel wametutoa kimasomaso Watanzania baada ya video yao ya wimbo wa Game walioshirikiana na Vanessa Mdee kushika namba nne katika chat ya video 50 bora za MTV Base Africa zilizofanya vizuri mwaka 2015..

Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana umeshika namba 5 katika chat hizo, wimbo huo wa Nana pia umetengenezwa na producer Nahreel kitu kinachomfanya aendelee kuwa producer bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania na East Africa kwa ujumla,

Mwimbaji Wizkid wa Naigeria Ameshika Namba 6.

Pongezi ziende kwao @nahreel,@aikanavykenzo wanaounda kundi la Navykenzo
pia pongeze kwa Diamond Platnumz kwa kuwa namba 5 katika chat hiyo...

Mwaka huu tegemea mambo makubwa kutoka kwao na The Industry kwa ujumla.

Saturday, January 02, 2016

Usafiri wa treni wasitishwa kwa muda kutokana na eneo la Kilosa na Gulwe kukumbwa na mafuriko

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia jana Januari 01, 2016, huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko.
Kwa mujibu wa taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako eneo la mafuriko kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe.
Kutokana na uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119 . wa treni hiyo.
Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana, safari zote kuanzia jana Januari 01, 2016, kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala.
Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara zitaanza tena. Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
Dar es Salaam,
Januari 02, 2016

Mazoezi ya Kitaifa ya Bonaza la Matembezi ya Wanamichezo wa Zanzibar Uwanja wa Amaan Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akishiriki katika Matembezi ya Bonaza la Wanamichezo wa Zanzibar akiongoza matembezi hayo yalioazia katika viwanja vya Matumbnaku Miembeni na kumalizia katika viwanja vya Amaan Zanzibar kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Abdalla Mwinyi Khamis, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Shariff Khamis Raiswa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Mwenyekiti wa Umoja Mazoezi Zidi , Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Bihindi Hamad, Waziri wa Kilimo na Mali Asili Mhe Sira Ubwa Mwaboya na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B Ayoub Mohammed Mahmoud. Picha zote na OthmanMapara.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akipokea matembezi ya Wanamichezo mbalimbali walioshiriki matembezi hayo ya Kitaifa ya Bonaza la Michezo Zanzibar yaliowashirikisha Wanamichezo kutoka Ungua Pemba na Dar es Salaam wakiingia katika viwanja vya Amaan kumalizia matembezi hayo na kumalizia katika viwanja vya Amaan Zanzibar kwa ajili ya mazoezi ya viungo.

Kitabu kinachoelezea safari ya kimaisha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli chakamilika

Heri ya mwaka mpya. Nina furaha kuwafahamisha kuwa kitabu kipya, "Dokta John Pombe Magufuli: Safari ya Urais, Mafaniko na Changamoto katika Urais wake" sasa kinapatikana. Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu kadhaa ninavyotarajia kuvichapisha mwaka huu 2016. 

Wakati kitabu hiki kikiingia sokoni, kitabu kingine kuhusu taaluluma ya Usalama wa Taifa kipo katika hatua za mwisho, na matarajio ni kukiingiza sokoni mwishoni mwa mwezi huu.

Kitabu hiki cha Dokta Magufuli kina sura sita. Katika utangulizi, kitabu kinazungumzia mazingira ya uchaguzi mkuu uliopita, msisitizo ukiwa kwenye hali ya nchi ilivyokuwa kabla ya uchaguzi huo.

Kadhalika, utangulizi huo unaelezea mabadiliko ya ghalfa ya kisiasa, hususan ndani ya CCM, yaliyojitokeza kufuatia jina la mwanasiasa aliyekuwa maarufu kuliko wote wakati huo, Edward Lowassa, kukatwa na chama hicho tawala wakati wa mchakato wa kupata mgombea wake wa kiti cha urais.

Sura ya kwanza inamtambulisha Dokta Magufuli, kwa kuangalia historia fupi ya maisha yake. Sura ya pili inaeleza mchakato aliopitia Dkt Magufuli hadi kuibuka mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Sura hii inachambua kwa undani ushindani miongoni mwa makada zaidi ya 40 waliochukua fomu kuwania urais kupitia chama hicho.

Hoyce Temu atembelea kituo cha Nunge kinacholea wazee na walemavu

IMG_9916 IMG_9920
Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (wa pili kushoto) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) kushoto Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye ( wa pili kulia), Katibu wa Kamati ya Miss Tanzania Bosco Majaliwa (kulia) pamoja na mpiga picha wa kipindi cha Mimi na Tanzania, Geofrey Magawa a.k.a KIM (kushoto) wakiwasili Desemba 31, 2015 kwenye makazi ya wazee na watu wenye ulemavu wasiojiweza yaliyopo Nunge, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Na Rabi Hume, Modewjiblog
Miss Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu amemaliza mwaka 2015 kwa kutembelea kituo Nunge ambacho ni makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza kilichopo Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam. Hoyce ambaye amekuwa akisaidia watu wa aina mbalimbali wenye matatizo ikiwa ni kama moja ya kazi wanazofanya mamiss kwa jamii pia kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho kimekuwa kikisaidia watu mbalimbali na katika halfa hiyo aliongozana na watu wake wa karibu ikiwepo kamati ya Miss Tanzania. Katika halfa hiyo iliyodhaminiwa na Malaika Beach, Hoyce baada ya kuwasili kituoni hapo yeye na timu nzima aliyoongozana nayo walifanya shughuli za kijamii katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika makazi ya wazee na walemavu wasiojiweza waliopo kituoni kwa kupulizia dawa za kuulia wadudu katika nyumba zao, kugawa dawa za mbu, maji, juice na biskuti na baadae wakapata chakula cha pamoja na wazee na walemavu wasiojiweza.

Akizungumzia halfa hiyo ya kufunga mwaka, Hoyce Temu alisema kumekuwepo na kusahaulika kwa makundi ya watu wasiojiweza na jinsi muda unavyokwenda wanazidi kusahaulika na jamii inayowazunguka. Alisema yeye kama Miss Tanzania ana wajibu wa kujitoa kuwasaidia watu wa aina hiyo na amekuwa akifanya maeneo mengi kwa kujumuika nao kwa kuwapa msaada na kuwafariji kwani nao wana thamani kama binadamu wengine. "Kadri inavyokwenda kumalizika karne ya 21 kunazidi kuongezeka kwa makundi ya wasiojiweza na mimi kama Miss Tanzania nimeamua kujitoa kwa kusaidia makundi haya kwani ni wajibu wetu na tukumbuke na sisi tunaelekea huko," alisema Hoyce.

Friday, January 01, 2016

Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa Mwanza atoa neno kwa Watanzania

Na"George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda Bunoro anawatakia Waendesha Pikipiki wote nchini Kheri ya Mwaka Mpya 2016 huku akiwasihi kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria na taratibu za Usalama barabarani bila shuruti.

"Tuache Mchezo na Vyombo vya Moto, Tuvae Elmenti, tusibebe mishkaki (zaidi ya abiria mmoja) tusiendeshe kwa mwendo kasi kwani ni hatari, tusitumie pombe tukiwa kazini huku tikiwapenda abiria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vya aina yoyote". Anasema Bunoro.

Aidha Bunoro amewaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kwa namna moja ama nyingine kutokana na kazi ya bodaboda na kwamba kusameheana ndilo jambo la msingi huku akiwakumbusha bodaboda  kujipanga katika majukumu yao ili kuendana na kasi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya 'Hapa Kazi Tu'.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...