https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Sunday, August 03, 2014

Habari za hivi punde, Michael Wambura afukuzwa uanachama wa klabu ya Simba



HATIMAE Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania FAT sasa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Wambura, ametimuliwa kuwa mwanachama wa klabu ya Simba, kwa tuhuma za kuipeleka klabu yake mahakamani.

Chiku Gallawa mgeni rasmi Handeni Kwetu Foundation



NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, pichani chini, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa taasisi ya Handeni Kwetu Foundation, utakaofanyika kesho Jumanne, katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
 Tukio hilo la uzinduzi wa taasisi hiyo limepangwa kuanza saa 10 za jioni ambapo wamealikwa wageni mbalimbali kwa ajili ya kuitambulisha kabla ya kuanza kazi zake rasmi nchini Tanzania.

Akizungumzia hilo, jijini Dar es Salaam, Msemaji wa taasisi hiyo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wameona wamualike RC Gallawa kuwa mgeni rasmi kwakuwa ni miongoni mwa viongozi makini na wenye kiu ya maendeleo hapa nchini.

Alisema kuwa kitendo cha kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa Tanga, kinaonyesha namna gani viongozi wa serikali wanashirikiana na wadau wote kwa ajili ya kufanikisha mipango ya kimaendeleo.

“Tanzania imejaliwa kuwa na viongozi makini mno, hivyo taasisi imemualika Mheshimiwa Gallawa kuwa mgeni wake rasmi ili ashirikiane na wageni waalikwa kuitambulisha taasisi.

“Tunaamini kwa pamoja tutafanikisha kuitambulisha taasisi kwa wadau wote, hususan Watanzania kwa kupitia Handeni Kwetu Foundation, ukizingatia kuwa imesajiliwa kufanya kazi zake nchini nzima,” alisema.

Kwa mujibu wa Mbwana, sera na mikakati ya taasisi hiyo itaanikwa katika utambulisho huo utakaokuwa na malengo mahususi ya kujikwamua kiuchumi na kuhamasisha masuala ya utawala bora.


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...