https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, February 28, 2013

TIFU TIFU: Michael Wambura azidi kumng'ang'ania Tenga kwa kumtaka aitishe Uchaguzi Mkuu wa TFF haraka


Umemuona jamani Tenga?? Hapa anawaonyesha wanahabari gazeti lilioandika habari za kujiuzulu kwake mwaka 2001....
 

Na Rahimu Kambi, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka TFF sasa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Wambura, amesema endapo Tanzania itafungiwa na Shirikisho la Mpira la Dunia (FIFA), wa kustahili kulaumiwa ni Leodgar Tenga, Rais wa Shirikisho hilo.

Wambura alimataka Tenga aitishe mkutano badala ya kufurahia ujio wa viongozi wa FIFA, ikiwa ni njia ya kutaka Tanzania ifungiwe jambo ambalo likitokea, Watanzania watalia na Rais huyo aliyemaliza vibaya muda wake wa mwisho.

Aidha, Wambura aliitaka TFF na Kamati zake zote kuwa ziitishe Uchaguzi Huru, kabla ya kumaliza muda wake kwa mujibu wa sheria, huku akisema kuwa uamuzi wa serikali unapaswa kuungwa mkono maana umekuja kumaliza tatizo, hivyo wanaona kuwa Tanzania itafungiwa basi wa kulia naye ni Tenga.

Baada ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kutangaza kutoitambua Katiba ya TFF ya mwaka 2012, Tenga aliitisha kikao cha Kamati ya Utendaji kinachotarajiwa kufanyika mwisho mwa wiki.

Michael Wambura, akionyesha kipande cha gazeti kwa wanahabari, ambalo mwaka 2001 liliandikwa juu ya kujiuzulu kwa Leodgar Tenga Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), wakati huo ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kama ushahidi wa kigeu geu chake anapokuwa kwenye uongozi.....
 

Waziri wa Nishati na Madini Professor Sospeter Muhongo alipotembelea Makao Makuu ya Kampuni ya BG Uingereza


Makao makuu ya Kampuni ya BG.
Mh waziri Muhongo akisalimia na CEO wa BG Chris.
Mh Waziri akitembelea makao makuu ya BG Group.

TAARIFA YA MKUTANO MKUU WA WADAU WA PSPF KUFANYIKA MACHI 7 NA 8 JIJINI DAR ES SALAAM

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
TAARIFA KWA UMMA
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unawajulisha kwamba Mkutano Mkuu wa wadau utakaofanyika tarehe 07 na 08 Machi 2013 kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi jioni katika Ukumbi wa JB Belmont uliopo ghorofa ya 6 ya Jengo la Maegesho la PSPF - Golden Jubilee Towers , Dar es Salaam.

Madhumuni ya Mkutano huu ni kutoa taarifa ya hesabu ya mwaka na utendaji wa Mfuko na kutathmini mafanikio na changamoto zinazoukabili Mfuko na Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa ujumla.
Tafadhali thibitisha ushiriki wako kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Makao Makuu, Dar es Salaam au Ofisi za PSPF mikoani kabla ya tarehe 05 Machi 2013.

“PSPF - Tulizo la Wastaafu”
 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma,
Golden Jubilee Towers, Ghorofa ya 6-13, Mtaa wa Ohio/Kibo,
Central Area, Kiwanja Na. 8, 9, 12 na 15, S. L. P 4843. Dar-es-Salaam.
Simu: +255 22 2120912/52 au +255 22 2127375 /6
Nukushi: +255 22 2120930.
Zawadi za Mashindano ya Mpinga Cup zatangazwa


IMG_7090

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari leo katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, wakati alipotangaza zawadi za washindi wa kombe la Mpinga Cup linaloshirikisha waendesha Bodaboda katika mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.
IMG_7228
 
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akionyesha moja ya jezi zitakazotumika katika michuano ya mpinga cup itakayoanza leo jijini Dar es saalam chini ya udhamini wa Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani
………………………………………………
Kiongozi mkuu maandalizi ya Mashindano ya Mpinga Cup ametangaza zawadi mbalimbali zitakazotolewa kwa timu zitakazoshiriki katika michuano ya Mpinga Cup inayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodabado wa jijini dar esa saalam yanayotegemea kufanyika leo katikaviwanja vya Oysterbay police kwa muda wa wiki moja.

Akitangaza zawadi hizo ASP Emilian Kamwanda ambaye ni msaidizi Mwandamizi wa polisi na Kiongozi wa maandalizi ya michuano ya mpinga cup alisema” leo tunayo furaha kutangaza zawadi mbalimbali za washindi katika mashindano hayo ambayo yana lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikiki (bodaboda). Na zawadi hizi ziko kama ifuatavyo.

Mshindi wa kwanza atapata Kombe, Pesa taslimu shilingi million moja, jezi set moja, kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1, mshindi wa pili atapata pesa taslimu shilingi laki tano, jezi seti moja , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1 na mshindi wa tatu atapata pesa taslimu shilingi laki tatu, , kofia ngumu (helmet) 15 pamoja na mpira 1.

Aidha zawadi zitatolewa kwa Mchezaji bora na Goalkeeper bora ambapo kila mmoja atapata pesa taslimu shilingi laki moja, vocha za kufanya manunuzi Mr Price zenye thamani ya Laki moja na kofia ngumu (helmet) 1
Timu tano zitakazoshindwa pia hazitaondoka hivihivi , zitazawadiwa kila moja mipra na kofia ngumu Helmet.

Mashindano ya Mpinga Cup yameandaliwa na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani na kudhaminiwa na Airtel, Rotary club, Mr.Price, Home Shopping Center pamoja na Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, ili kutoa elimu kwa waendesha pikipiki juu ya sheria mbalimbali za usalama , kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii.

Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe leo katika viwanja vya Polisi Oysterbey kwa kushirikisha timu 8 za waendesha pikipiki. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.

MKOA WA RUVUMA WAWAKUMBUKA MASHUJAA WALIO KUFA KWA KUNYONGWA WAKATI WA VITA VYA MAJIMAJI MWAKA 1906, JANA

Waziri wa Maliasili na Utalii Nchini Tanzania Balozi Hamis Kagasheki ameweza kuongoza Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma katika kuwakumbuka Mashujaa wa Vita vya Majimaji walionyonga tar 27/02/1906 na Wajerumani ambapo Mashujaa 61 walizikwa katika Kaburi moja.
  1. Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma hukumbuka Mateso waliyoyapata Babu zao, Hapo wapo katika Viwanja vya Mashujaa Mahenge Manispaa ya Songea kushuhudia Maombolezo yaliyoongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Kagasheki.
Uwanja wa Mashujaa Mahenge umezungukwa na picha za Mashujaa wa Vita vya Majimaji hiyo ni picha ya shujaa Chifu Songea Mbano

Wednesday, February 27, 2013

TANGAZO LA HANDENI KWETU

TANGAZO
Asante kwa kutuunga mkono. Tunaomba uendelee kuwa pamoja na sisi.

EWE mdau wa Handeni Kwetu Blog, pia unaombwa kuiunga mkono group la Handeni Kwetu ambalo ni ndugu na blog hii kwa lengo lile lile la kuelimisha na kupeana habari kwa ujumla.

Ukishangia kwenye facebook, Andika Handeni Kwetu na utajiunga moja kwa moja ili tuendelee kuwa na muungano mkubwa, hata kama wewe sio mtu mwenye asili ya Handeni, bado una nafasi yako kama Mtanzania.

Kujiunga kwenye group hilo, tutaendelea kuwa kwenye juhudi za kutafuta namna gani ya kujadiliana mambo kwa mapana zaidi. Angalizo. Group la Handeni Kwetu kwenye mtandao wa kijamii wa facebook halipo kwa ajili ya watu wa Handeni tu, bali Watanzania wote.

Bila kuangalia wapi tulipozaliwa, tunapoishi, ni wakati wetu ku-join kwa ajili ya kuleta mwangaza zaidi kwa maendeleo ya Taifa. Jinsi ya kujiunga.

Kama wewe tayari upo kwenye facebook, ingia kwenye Search for peole, places and things na kuandika kwa herufi kubwa HANDENI KWETU, kasha bonyeza hapo na kufuata utaratibu wa kujiunga na kuwa mdau wa group hilo.

ASANTE kwa kuwa mdau wa blog ya Handeni Kwetu, huku tukiahidi kwa pamoja kukuletea habari moto moto kwa namna moja ama nyingine.

Kwa maoni na ushauri, tuandkie kwa email ya kambimbwana@yahoo.com au +255 712 053949
 






Waziri wa Nishati na Madini Mh. Sospeter Muhongo alipata fursa kuongea na Watanzania waishio Uingereza katika mwaliko rasmi kutoka serikali ya Uingerza. Katika ziara yake nchini Uingereza Mh Sospeter Muhongo ameambatana na Bw. Athanas Macheyeki, Bw. Seleman Hatibu na Bw. Sosthenes Massola.

Mh. Muhongo aliwaeleza Watanzani suala zima la gas na jinsi gani serikali itavyotumia gas hiyo kuleta maendeleo ya nchi. Amesema “serikali itahakikisha kuwa kila kijiji kinapata umeme na mpaka kufikia mwaka 2025 nchi ya Tanzania itaondoka na umasikini”. 

Aliendelea kusema kuwa bila ya umeme hatutoweza kutoa umasikini hivyo wizara yake itatafuta miundo mbinu ya kisasa ili kuwezesha suala zima la matatizo ya umeme linaondoka. Pia amesema wizara yake itaangalia tena ufumo wa Tanesco na kuanzisha idara zingine ambazo zitashirikiana na zitawezesha kutatua matatizo yanayoikabili Tanesco.

Vilevile Mh Muhongo aliwataka wawekezaji wa Kitanzania waweze kuwekeza katika sekta ya nishati na madini.

Habari na Ally Muhdin- London



Mh. Balozi Peter Kallaghe

TANGAZO LA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TAWI LA CCM DMV

Email address:ccmwashdc@gmail.com
Ndugu Wana CCM DMV mnaombwa kuhudhuria mkutano wa uchaguzi bila kukosa,
Ni nafasi ya kuwachagua viongozi wako utakao wapenda kujenga Chama imara.
SIKU: JUMAMOSI Machi 16, 2013
MUDA: SAA 10 JIONI (4pm)

MAHALI: TUTAWATANGAZIA
Ili uweze kupiga kura hakikisha una kadi yako ya Chama na uwe mwanachama hai, na kama huna kadi au umepoteza tafadhali wasiliana na Katibu wa Tawi wa muda
Yacob Kinyemi, Simu (202)-629-7841, email: yacob1972@yahoo.com
Nafasi zinazowaniwa ni:
1) Mwenyekiti wa tawi
2) Katibu wa Tawi
3) Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wa Tawi
4) Katibu wa Fedha na Uchumi wa tawi
5) Mwenyekiti wa Vijana wa Tawi (UVCCM)
6) Katibu wa Vijana wa Tawi (UVCCM)
7) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT)
8) Katibu wa Jumuiya ya Wanawake ya Tawi (UWT)
9) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Tawi
10) Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Tawi
SIFA ZA MGOMBEA:
1. Awe na umri kuanzia miaka 18
2. Awe mwachama wa CCM mwenye kadi
Fomu za kugombania nafasi za uchaguzi ziwakilishwe kwa M/Kiti ( HIDAYA MAHITA)wa Kamati ya
Uchaguzi kwa njia ifuatayo:
Fax: 1(888)835-5784 Email: ccmwashdc@gmail.com
Mailing address: 1709 HAMPSHIRE GREEN LANE#33 SILVER SPRING MD 20903
MWISHO WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU HIZO NI TAREHE 8 MARCH 2013

Extra Bongo yajivunia watatu wake wapya



Nadine Conpresor, mcheza shoo mpya wa Extra Bongo akionyesha umahiri wake, mbele ya repa wake, Papy Catalogue.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, jana iliwatambulisha wanamuziki watatu, akiwamo Papy Catalogue repa aliyewahi kufanya kazi na FM Academia, Nadine Conpresor, mnenguaji aliyetoka Akudo Impact na Adam Mbombole, mwimbaji kutoka K-Mondo Sound zote za jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Ally Choki, alisema kwamba kuwatambulisha wanamuziki hao ni ishara ya kuboresha na kuiweka juu zaidi katika kipindi chote cha muziki wa dansi nchini.

Dawa zaadimika Hospitali ya Wilaya Kilwa



Mkuu wa Wilaya Kilwa, Abdallah Ulega.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HOSPITALI ya Wilaya ya Kilwa imelalamikiwa na wananchi wilayani humo kwa kukosa dawa, hali inayowapa wakati mgumu wagonjwa wanaopelekwa hapo kupata matibabu, huku dawa pekee inayopatikana ikiwa ni Panadol.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao, baadhi ya wananchi wa wilayani Kilwa walisema kuwa kukosekana kwa dawa kwenye hospitali hiyo kunasababisha watu waishi kwa tabu, huku wengine wakipata madhara makubwa zaidi.

Alisema mara kwa mara majibu yanayotolewa  na viongozi kwenye hospitali hiyo ni kukosekana kwa dawa, jambo ambalo kwa wananchi wanaotegemea uwepo wa hospitali ya serikali kunawaweka kwenye wakati mgumu.

Akizungumzia taarifa hizo kwa njia ya simu, Mkuu wa wilaya wa Kilwa, Abdallah Ulega, alisema matatizo ya dawa kwenye hospitali ya wilaya yake si habari ngeni, huku akisema kukosekana huko wakati mwingine ni kuchelewa kufika kwa fedha za kununulia dawa.

Alisema kuwa juhudi zinazofanywa na serikali ya wilaya ni kufanya mazungumzo na wanaoshughulia na usambazaji wa dawa, ambao ni Bohari Kuu ya Dawa (MSD), ili kutatua changamoto ya ukosefu wa dawa katika Hospitali hiyo.

“Hospitali nyingi katika baadhi ya wilaya zetu zinaweza kufikwa na upungufu wa dawa, maana kabla ya kufika, kunakuwa na mizunguuko ya hapa na pale, ingawa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wake wanaishi vizuri na kupata matibabu.

“Kwa pamoja tutaliangalia suala hilo na kufanya kazi kwa nguvu zote kuwahadumia Watanzania, wakiwamo wa wilayani Kilwa kwa kusimamia vyema na kushauri au kutoa taarifa inapofikia suala la kukosekana kwa dawa za aina yoyote ile katika hospitali zetu,” alisema.


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...