https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, January 04, 2013

Yanga kuwavaa Bielefeld Uturuki kesho



Yanga wakiwa mazoezini nchini Uturuki

Na Baraka Kizuguto, Uturuki
Timu ya Yanga kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo utakaofanyika mjini Antalya, nchini Uturuki, kuanzia saa 10 za jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Yanga imeweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya huku ikifanya mazoezi tangu siku ya jumatatu na wachezaji wote wameonekana kufurahia mazingira ya kambi na huduma zote kwa ujumla.

Baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku tano (5) mfiululizo itatumia mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Arminia Bielefed kama kipimo tosha cha maendeleo ya mafunzo yanayoendelea nchini Uuturuki.

Kocha wa timu hiyo, Mholanzi, Ernie Brandts, amesema anashukuru wachezaji wake wapo vizuri kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.

Aidha Brandst alisema anajua mchezo wa kesho utakua mgumu kwakuwa Arminia Bielefeld ni timu nzuri na imekuwa ikishiriki Ligi Kuu ya Ujerumani mara kadhaa.


No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...